Pata taarifa kuu

Guterres atoa wito kwa Israel 'kuondoa vizuizi kwa ajili ya msaada' kwa Gaza inayotishiwa na njaa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa ziarani nchini Misri, ametoa wito kwa Israel siku ya Jumapili, "kuondoa vikwazo kwa ajili ya msaada" kwa Ukanda wa Gaza unaotishiwa na njaa, na kuzitaka Israel na Hamas "kusitisha mapigano mara moja".

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitembea na Gavana wa Sinai Kaskazini Meja Jenerali Mohamed Abdel-Fadel Shousha, kwenye uwanja wa ndege wa Al Arish, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la Kiislamu la Palestina Hamas, nchini Misri Machi 23, 2024.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitembea na Gavana wa Sinai Kaskazini Meja Jenerali Mohamed Abdel-Fadel Shousha, kwenye uwanja wa ndege wa Al Arish, huku kukiwa na mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la Kiislamu la Palestina Hamas, nchini Misri Machi 23, 2024. REUTERS - Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Baada ya karibu miezi sita ya vita, Bw. Guterres alishtumu, wakati wa ziara yake upande wa Misri kwenye eneo la mpakani na Palestina linalozingirwa, maumivu ya Wapalestina, wafungwa wa "uhasama usio na mwisho".

"Unapoiangalia Gaza, ni kama vile milima yote ya dunia imeiangukia, na hivyo kuchochea vita, njaa, uvamizi na njaa", amesema Bw. Guterres wakati wa mkutano wa pamoja na Waziri wa mambo ya Nje wa Misri Sameh Choukri na vyombo vya habari. "Ulimwengu unaona kwamba ni wakati sasa wa vita kukoma na kufikiria kusitisha mapigano mara moja", ameongeza

Mapema siku ya Jumapili, alikutana na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi, akiambatana na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), Philippe Lazzarini. Karibu miezi sita ya vita vibaya ambavyo viliutumbukiza Ukanda wa Gaza Β katika hali mbaya ya kibinadamu.

Bw. Guterres amekaribisha "jukumu muhimu la kisiasa na kibinadamu la Misri pamoja na uwanja wa ndege wa Al Arish na kituo cha mpakani cha Rafah, maeneo muhimu kwa kuingiza misaada muhimu huko Gaza".

Nchi ya kwanza ya Kiarabu kuitambua Israel, Misri ni mpatanishi wa jadi kati ya Israeli na Palestina. Pamoja na Qatar, ilichangia kuanzishwa kwa usuluhishi ambao uliwezesha kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wa Kipalestina mwishoni mwa mwezi Novemba.

Vita hivyo vilianza Oktoba 7 baada ya shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la Hamas katika ardhi ya Israel ambalo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 1,160, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la hbari la AFP kutoka vyanzo rasmi vya Israeli. Kulingana na vyanzo hivi, karibu watu 250 walitekwa nyara na 130 kati yao bado ni mateka huko Gaza, 33 kati yao wanaaminika kufariki. Katika kulipiza kisasi, Israel iliapa kuwaangamiza Hamas walioko madarakani Gaza tangu mwaka 2007. Jeshi lake lilianzisha mashambulizi ambayo yalisababisha vifo vya watu 32,226 huko Gaza, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.