Pata taarifa kuu

Gaza: Mawaziri watano wa Kiarabu wakusanyika Cairo kabla ya kukutana na Blinken

Misri, Qatar, Saudi Arabia, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu zimeshiriki katika mkutano wa mawaziri kuhusu vita huko Gaza siku ya Alhamisi huko Cairo, kabla ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kulingana na diplomasia ya Misri.

Baada ya kuanza kwa vita Oktoba 7 kati ya Israel na Hamas, Marekani ilipiga kura ya turufu maazimio kadhaa ya kutaka kusitishwa kwa vita katika mzozo huu uliochochewa na shambulio la Hamas nchini Israel.
Baada ya kuanza kwa vita Oktoba 7 kati ya Israel na Hamas, Marekani ilipiga kura ya turufu maazimio kadhaa ya kutaka kusitishwa kwa vita katika mzozo huu uliochochewa na shambulio la Hamas nchini Israel. © SAID KHATIB/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbali na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo tano, pia aliyeshiriki katika mkutano huo ni Hussein al-Sheikh, afisa mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, karibu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, ameandika msemaji wa diplomasia ya Misri Ahmed Abou Zeid kwenye X.

Viongozi hawa "wamejadili juhudi zinazohitajika kusitisha vita vya Israel, kufikia usitishaji vita huko Gaza na kuhakikisha kufikishwa kwa misaada yote ya kibinadamu" katika eneo la Palestina ambako Umoja wa Mataifa unahofia njaa inayokaribia baada ya miezi mitano zaidi ya vita, ameongeza.

Baadaye, watakutana na Bw. Blinken ambaye tayari amejadiliana na mwenzake wa Misri Sameh Shoukri na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi "juhudi za kuwalinda raia wa Palestina" na njia za "kufanikisha usitishaji mapigano mara moja ikiwa ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka.

Bw. Blinken aliviambia vyombo vya habari vya Saudia siku ya Jumatano kwamba Marekani iliwasilisha rasimu ya azimio kwa wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayotaka "kusitishwa mara moja kwa mapigano yanayohusiana na kuachiliwa kwa mateka" huko Gaza.

Baada ya kuanza kwa vita Oktoba 7 kati ya Israel na Hamas, Marekani, mshirika mkuu wa Israel, alipiga kura ya turufu maazimio kadhaa ya kutaka kusitishwa kwa vita katika mzozo huu uliochochewa na mashambulizi ya Hamas nchini Israel.

Lakini kwa kuwa karibu watu 32,000 wamekufa huko Gaza kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Hamas na hatari ya njaa katika eneo la Palestina lililozingirwa, Marekani inasema inaongeza maradufu juhudi zake za usuluhishi. Kando na ziara ya Bw. Blinken, mazungumzo yalianza tena Jumatano mjini Doha kupitia wapatanishi wa Marekani, Qatar na Misri.

Mpango unaojadiliwa nchini Qatar utamaliza mapigano kwa muda huku mateka wa Israel wakibadilishana na wafungwa wa Kipalestina na utoaji wa misaada ya kibinadamu utaongzwa.

Siku ya Jumatano, afisa wa Hamas alisema jibu la Israel kwa pendekezo la kundi lake la kusitisha mapigano lilikuwa "hasi kwa ujumla" na linaweza "kuongoza mazungumzo kuelekea mkwamo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.