Pata taarifa kuu

Mfalme Abdullah II wa Jordan ashiriki katika zoezi la kudondosha misaada Gaza

Mfalme wa Jordan Abdullah ameshiriki katika utoaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza, shirika la utangazaji la umma la Al Mamlaka limetangaza siku ya Jumapili.

Mfalme Abdullah II wa Jordani, katika Baraza la Wawakilishi huko Amman, Machi 23, 2021.
Mfalme Abdullah II wa Jordani, katika Baraza la Wawakilishi huko Amman, Machi 23, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Video inamuonyesha mfalme huyo akiwa amevalia sare ya jeshi akipanda ndege ya kijeshi katika dhamira ya hivi punde zaidi ya Jeshi la Wanahewa la Jordan la kupeleka vifaa vya dharura vya matibabu katika hospitali inazosimamia katika eneo hilo lililokumbwa na vita. shrika hili la utangazaji halikubainisha tarehe zoezi hilo lilifanyika.

Misri yaonya kuhusu "athari" ya shambulio la Rafah

siku ya Jumapili, Misri imeonya juu ya "athari" ya uwezekano wa shambulio la kijeshi la Israel kwenye mji wa kusini wa Gaza wa Rafah, karibu na mpaka wake. "Misri imetoa wito kwa haja ya kuunganisha juhudi zote za kimataifa na kikanda ili kuzuia mji wa Palestina wa Rafah kulengwa," Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imeongeza katika taarifa.

Mamia ya watu huko Strasbourg waandamana kutaka kuachiliwa kwa mateka wa Hamas

Mamia ya watu wameandamana mjini Strasbourg, nchini Ufaransa siku ya Jumapili kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka wa Hamas na kupinga chuki dhidi ya Wayahudi. "Bado tunatumai kuachiliwa kwa mateka. Tumeshangazwa na mlipuko wa chuki dhidi ya Wayahudi. Lazima tuone mapambano dhidi ya Uislamu hadi mwisho, kwa ajili ya kuendelea kuishi,” amesema Pierre Haas, rais wa shirika la Crif Est.

Waandamanaji hao, ambao walikuwa 750 kwa mujibu wa polisi, wameandamana kutoka Uwanja wa Jamhuri hadi kwenye Sinagogi Kuu la Amani, bendera za Israel na Ufaransa mikononi. Kwenye barbara mbele ya Sinagogi, wamewasha mishumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.