Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Anthony Blinken anatarajiwa Mashariki ya Kati

Jeshi la Israel limeshambulia kwa makombora Ukanda wa Gaza ambapo makumi ya watu wanahofiwa kuuawa leo Jumapili, Februari 4. Hofu inazidi kuongezeka kutokana na uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kijeshi dhidi ya mji wenye msongamano wa watu wa Rafah, ambao ni makazi ya zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia makazi yao. Hamas inasema inahitaji muda zaidi kufikiria pendekezo la kusitisha mapigano mara ya pili katika vita vyake na Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu akiwa pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani wanahudhuria mkutano na wanahabari, mjini Doha, Qatar, Januari 7, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu akiwa pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani wanahudhuria mkutano na wanahabari, mjini Doha, Qatar, Januari 7, 2024. © Evelyn Hockstein / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Unachotakiwa kufahamu:

■ Wanajeshi wa Marekani na Uingereza walifanya mashambulizi dhidi ya maeneo 36 ya Wahouthi nchini Yemen siku moja baada ya mashambulizi ya Marekani nchini Iraq na Syria kuwalenga Walinzi wa Mapinduzi ya Iran.

■ Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa katika Mashariki ya Kati siku ya Jumapili kuunga mkono mazungumzo juu ya mapatano mapya kati ya Israel na Hamas. Atafanya ziara yake hadi Qatar, Misri, Israel, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na nchini Saudi Arabia.

■ Kusitishwa kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza na kubadilishana kwa mateka na wafungwa wa Kipalestina kutazingatiwa. Siku ya Jumamosi afisa mkuu wa Hamas alisema kuwa Israel inachelewesha makubaliano, wala haitaki kusitishwa kwa mapigano.

■ Mashambulizi ya angani yamelenga Rafah, hofu inaongezeka juu ya uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya jiji hili lenye watu wengi, kwenye mpaka uliofungwa na Misri. Zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia makazi yao, wanaotishiwa na uhaba wa chakula na magonjwa ya milipuko, sasa wamejaa katika makazi na kambi za muda.

■ Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Afya ya Hamas, Ijumaa Februari 2, watu 27,365 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Watu zaidi ya 66,630 wamejeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.