Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Israel yatekeleza mashambulizi ya anga kusini mwa Gaza

Mji wa Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, umesalia, Alhamisi, Januari 25, kuwa kitovu cha mapigano kati ya jeshi la Israel na Hamas kutoka Palestina siku moja baada ya shambulio baya lililosababisha vifo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanayohifadhi watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita.

Jengo la UNRWA llinalowapa hifadhi watu waliohamishwa limeteketea kwa moto huko Khan Younès, Jumatano Januari 24, 2024.
Jengo la UNRWA llinalowapa hifadhi watu waliohamishwa limeteketea kwa moto huko Khan Younès, Jumatano Januari 24, 2024. AP - Ramez Habboub
Matangazo ya kibiashara

 

Unachopaswa kukumbuka:

■ Qatar, Misri na Marekani kwa sasa zinajaribu kupatanisha ili kufikia mapatano mapya, marefu zaidi huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa. Lakini katika rekodi iliyopatikana na kituo cha habari cha Israel cha 12, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema hana imani na jukumu la Qatar kuwa mpatanishi, nchi ambapo uongozi wa kisiasa wa Hamas unaendesha shughuli zake.

■ Siku ya Jumatano Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina huko Gaza (UNRWA), Philippe Lazzarini, alishutumu "ukiukaji wa wazi wa kanuni za msingi za vita", baada ya jeshi la Israel kutekeleza shambulio dhidi ya jengo la UNRWA huko Khan Younes ambalo lilisababisha vio vya watu "tisa"  na 75 kujeruhiwa”, kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo huko Gaza.

■ Kulingana na ripoti iliyotangazwa siku ya Jumanne Januari 23 na Wizara ya Afya ya Hamas, watu 25,700 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Wengi wa waliofariki ni wanawake, vijana na watoto. Zaidi ya watu 63,000 walijeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.