Pata taarifa kuu

Je, Hamas na Israel waelekea kwenye mapatano mapya ya kuachiliwa kwa mateka wote?

Israel imewapa Hamas, kupitia upatanishi wa Misri na Qatar, muda wa miezi miwili katika mapigano na uvamizi huko Gaza ili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka wote, tovuti ya Marekani ya Axios iliripoti Jumatatu jioni.

Watu waliojeruhiwa huko Khan Younes, wafikishwa katika hospitali ya Rafah, ambako mapigano yanapamba moto, Jumanne Januari 23, 2024.
Watu waliojeruhiwa huko Khan Younes, wafikishwa katika hospitali ya Rafah, ambako mapigano yanapamba moto, Jumanne Januari 23, 2024. AP - Hatem Ali
Matangazo ya kibiashara

 

Pendekezo hili halimaanishi kumalizika kwa vita huko Gaza, bali mapatano ya pili, baada ya yale ya wiki moja ambayo yaliruhusu kuachiliwa kwa mateka mia moja badala ya angalau wafungwa 240 wa Kipalestina waliofungwa jela nchini Israel.

  Pendekezo la Israel linatoa fursa ya kurejea nchini Israeli mateka walio hai na miili ya mateka waliofariki katika awamu kadhaa, ya kwanza ikiwa ni pamoja na wanawake na wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 60, kulingana na Axios. Hii itafuatiwa na wanajeshi wa kike, wanaume wenye umri wa chini ya miaka 60 lakini sio wanajeshi, wanajeshi wa kiume wa Israeli, kisha miili ya wanajeshi waliofariki wakiwa mikononi mwa Hamas.

Watu waliojeruhiwa huko Khan Younes, wafikishwa katika hospitali ya Rafah, ambako mapigano yanapamba moto, Jumanne Januari 23, 2024.
Watu waliojeruhiwa huko Khan Younes, wafikishwa katika hospitali ya Rafah, ambako mapigano yanapamba moto, Jumanne Januari 23, 2024. AP - Hatem Ali

Kama sehemu ya mpango huo, Israel na Hamas watalazimika kukubaliana mapema juu ya idadi ya wafungwa wa Kipalestina watakaoachiliwa kwa kubadilishana na kila mateka kulingana na kundi lao, Axios imeongeza.

Wakati wa mkutano wa Jumatatu na familia za mateka, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alizungumza juu ya "mpango" wa Israeli, huku akidai kuwa hawezi "kuelezea" kwa undani, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.