Pata taarifa kuu

Pakistan yafanya 'mashambulio dhidi ya maficho ya magaidi' nchini Iran usiku kucha

Pakistan imetangaza Alhamisi hii kwamba imefanya "mashambulio dhidi ya maficho ya magaidi" nchini Iran usiku kucha, baada ya shambulio la Iran katika eneo lake kuua watoto wawili.

Islamabad, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistani. Pakistan imetangaza siku ya Alhamisi, Januari 18, kuwa imefanya mashambulizi katika mkoa wa mpaka na Iran wa Sistan-Baluchistan.
Islamabad, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistani. Pakistan imetangaza siku ya Alhamisi, Januari 18, kuwa imefanya mashambulizi katika mkoa wa mpaka na Iran wa Sistan-Baluchistan. AFP - AAMIR QURESHI
Matangazo ya kibiashara

 

"Leo asubuhi, Pakistan imefanya mfululizo wa mashambulizi ya usahihi, yenye uratibu wa juu na hasa kulenga dhidi ya maficho ya magaidi katika mkoa wa Sistan-Baluchistan kusini mashariki mwa Iran, serikali ya Pakistan ilisema katika taarifa.

"Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan, imebainisha kuwa " magaidi kadhaa waliuawa”. Wanawake watatu na watoto wanne waliuawa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.