Pata taarifa kuu

Islamabad inasema watoto wawili wameuawa katika shambulio la Tehran

Nairobi – Pakistan inasema watoto wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio la nchi jirani ya Iran siku ya Jumanne.

China imetoa wito kwa nchi hizo mbili kuwa na utulivu kuzuia mzozo zaidi.
China imetoa wito kwa nchi hizo mbili kuwa na utulivu kuzuia mzozo zaidi. AP - Julia Zimmermann
Matangazo ya kibiashara

Iran ilisema ililenga vituo viwili vinavyohusishwa na kundi la wanamgambo la Jaish al-Adl, kwa mujibu wa shirika la habari lenye uhusiano na jeshi la nchi hiyo.

Pakistan kwa upande wake imetupilia mbali madai ya Iran, ikisema kitendo hicho ni haramu na ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa.

Iran imepiga marafuku kundi la Jaish al-Adl ambalo liliasisiwa mwaka wa 2012, kundi hilo limekuwa likitekeleza mashambulio nchini Iran katika miaka ya hivi karibuni.

Shambulio hilo limetokea baada ya Iran kurusha makombora dhidi ya kile ilisema ni makao makuu ya kijasusi nchini Syria na Iraq.

Mashambulio ya Iran yanaongeza zaidi mzozo unaoendelea katika ukanda wa Mashariki ya kati hawa wakati huu ambapo Israel ikiwa vitani na wapiganaji wa kundi la Hamas lenye makao yake huko Palestine.

Kando na Hamas, Israel pia inapigana na waasi wa Huthi kutoka nchini Yemen ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulio kwenye meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu.

China imetoa wito kwa nchi za Pakistan na Iran kuwa na utulivu ilikuzuia mzozo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.