Pata taarifa kuu

Jerusalem yakumbwa na maandalano ya kuunga mkono kuachiliwa kwa mateka wa Israel

Waandamanaji wamekusanyika Jerusalem Magharibi Jumamosi hii jioni. Wanakusudia kuongeza shinikizo kwa serikali ili ifanye kinachowezekana mateka wanaoshikiliwa na Hamas waweze kuachiliwa huru.

Maandalano ya kutaka kuachiliwa kwa mateka, huko Tel Aviv, Israel, Jumamosi hii, Desemba 30, 2023.
Maandalano ya kutaka kuachiliwa kwa mateka, huko Tel Aviv, Israel, Jumamosi hii, Desemba 30, 2023. AFP - AHMAD GHARABLI
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu wamekusanyika Kaisaria, karibu na nyumba ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Waandamanaji wanaomba Benjamin Netanyahu ajiuzulu mara moja. Waandamanji waliinua mabango yenye alama ya mkono uliojaa damu katikati ya neno "mhalifu," Gazeti la Haaretz limeripoti.

Maelfu ya watu pia wanaandamana katikati mwa Tel Aviv kutaka, kwa mara nyingine tena, mkuu wa serikali ajiuzulu.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel ilimwalika Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant na mjumbe wa baraza la vita Benny Gantz kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumamosi hii saa 8:30 usiku., lakini waziri huyo alitangaza kwamba hawatahudhuria, linaripoti Gazeti la Haaretz. Bw. Gantz anabaini kwamba mkutano huu hauna manufaa, hakuna kilichotokea kuhalalisha mkutano huo, kulingana na Haaretz. Kuhusu Bw. Gallant, hakutaka kuhudhuria mkutano huu wa waandishi wa habari bila Bw. Gantz.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.