Pata taarifa kuu

Wapalestina 165 wauawa na 250 kujeruhiwa ndani ya saa 24 zilizopita

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi, Desemba 30, kundi la Hamas kutoka Palestina limeripoti mapigano makali huko Khan Younes, mji mkuu wa kusini mwa Gaza, na katikati mwa eneo hili lililozingirwa, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mabaya ya anga katika eneo la Nuseirat. Raia wamelundikana kwenye "kiwanja kidogo kusini mwa eneo hilo, katika eneo la Rafah, mkuu wa operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ametangaza Ijumaa kwenye mtandao wa X.

Mpalestina akimtoa msichana aliyejeruhiwa katika eneo la mashambulizi ya Israel katika eneo la Al Zawayda, katikati mwa Ukanda wa Gaza, tarehe 30 Desemba 2023.
Mpalestina akimtoa msichana aliyejeruhiwa katika eneo la mashambulizi ya Israel katika eneo la Al Zawayda, katikati mwa Ukanda wa Gaza, tarehe 30 Desemba 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu:

■ Wakati wa usiku, kundi la Hamas kutoka Palestina limeripoti mapigano makali huko Khan Younes, mji mkuu wa kusini mwa Gaza, na katikati mwa eneo hili lililozingirwa, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mabaya ya anga eneo la Nuseirat.

■ Muda mfupi baada ya saa sita usiku siku ya Jumamosi, jeshi la Israel limetangaza mashambulizi nchini Syria, kulipiza kisasi kwa makombora yaliyorushwa kutoka nchi hii jirani, makombora ambayo yaliangukia katika maeneo ya mpakani yaliyo chini ya udhibiti wake.

■ Ujumbe wa Hamas uliwasili Cairo siku ya Ijumaa Desemba 29 ili kujadili uwezekano wa mpango wa kusitisha mapigano ambao pia unaotoa fursa ya kuachiliwa kwa mateka.

■ Afrika Kusini iliishutumu Israel mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa kujihusisha na "vitendo vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza", mahakama hiyo, chombo kikuu cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, ilitangaza siku ya Ijumaa.

■ Wizara ya Afya ya Hamas ilitangaza idadi mpya ya watu 21,672 waliouawa tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, na 56,165 kujeruhiwa. Watu 1,140 waliuawa katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, kulingana na data iliyotolewa na serikali ya Israeli. Jeshi la Israel lilisema Alhamisi kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 2,000 wa Kipalestina tangu kumalizika kwa mapatano ya usitishwaji wa mapigano mapema mwezi Desemba. Wanajeshi 167 wa Israel wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza Oktoba 27, kulingana na takwimu za hivi punde kutoka jeshi la Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.