Pata taarifa kuu

Israel yapambana katika 'vita vya pande nyingi,' waziri wa ulinzi asema

Jeshi la Israel linaendelea na mapigano huko Gaza siku ya Jumanne, Desemba 26, baada ya kutangaza Jumatatu kuzidisha mashambulizi yake yenye lengo la kuangamiza Hamas. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema amani itapatikana tu ikiwa eneo hilo "litapokonywa silaha" na "kuwatimua watu wenye itikadi kali".

Ukanda wa Gaza, Desemba 26, 2023.
Ukanda wa Gaza, Desemba 26, 2023. © VIOLETA SANTOS MOURA / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kujua:

■ Jeshi la Israelilimeendesha mashambulizi mapya siku ya Jumanne. Kambi ya wakimbizi ya Nur Shams, lakini pia nyumba na eneo linalozunguka hospitali ya Nasser katika mji wa Khan Younes zimelengwa na mashambulizi hayo.

■ Katika Ukanda wa Gaza, mawasiliano ya simu za mezani na intaneti yamekatwa tena siku ya Jumanne.

■ Baada ya kuzuru Gaza, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza kuizidishwa kwa mapigano na kukadiria kuwa amani itapatikana tu ikiwa eneo la Gaza "litapokonywa silaha" na "kuwatimua watu wenye itikadi kali".

■ Wizara ya Afya ya Hamas ya Palestina imetangaza siku ya Jumanne, Desemba 26, kwamba operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza zimesababisha vifo vya watu 20,915 tangu kuanza kwa vita Oktoba 7, na zaidi ya watu 54,918 kujeruhiwa. Watu 1,140 waliuawa katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, kulingana na data iliyotolewa na serikali ya Israeli. Siku ya Alhamisi jeshi la Israel lilisema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 2,000 wa Kipalestina tangu kumalizika kwa usitishwaji vita mapema mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.