Pata taarifa kuu

Amnesty International: 'Hakuna mateka atakayeachiliwa' bila kusitishwa kwa mapigano huko Gaza

Tangu tarehe 7 Oktoba na mashambulizi ya umwagaji damu ya Hamas katika ardhi ya taifa la Israel, jeshi la Israel limekuwa likishambulia Ukanda wa Gaza bila kuchoka, na kusababisha maelfu ya wahanga wa raia kwa mujibu wa kundi la Hamas lililo madarakani katika eneo la Palestina. Hali hii inafanya "kutowezekana" kuachiliwa kwa mateka 240 ambao bado wanashikiliwa huko Gaza , kulingana na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International.

Agnès Callamard,mwakilishi wa Amnesty International.
Agnès Callamard,mwakilishi wa Amnesty International. © RFI/Véronique Gaymard
Matangazo ya kibiashara

 

"Njia bora ya kujadili kuachiliwa kwa mateka hawa ni kuifanya ndani ya mfumo wa usitishaji mapigano. Hakuna mateka atakayeachiliwa katika mfumo huu wa sasa," ametahadharisha Agnès Callamard kwa mujibu wa BFMTV.

Israeli inakataa "maafikiano yoyote ya usitiswaji wa mapigano kwa muda"

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Ijumaa kwamba amekataa "makubaliano ya muda bila kuachiliwa kwa mateka" waliotekwa nyara mnamo Oktoba 7.

Muda mfupi kabla, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema amejadiliana na Benjamin Netanyahu uwezekano wa "kusitishwa kwa mapigano kwa ajili ya kutoa nafasi kwa misaada ya kibinadamu" katika mzozo kati ya Israel na Hamas, ili kuwalinda raia wa Palestina na kuongeza usambazaji wa misaada kwa wakazi milioni 2.4 chini ya mashambulizi ya Israel.

"Hakuna pa kukimbilia. Hakuna sehemu ambayo ni salama," mwakilishi wa Amnesty International amesema.

Kisha ameshutumu "adhabu ya pamoja" iliyotolewa na jeshi la Israel kwa wakazi wa Palestina, ambayo inaweza kuchukuliwa kama "uhalifu wa kivita".

Kulingana mwakilishi wa Amnesty International, mashambulizi ya kigaidi ya Hamas, ambayo Amnesty International inalaani vikali, "sio sababu tosha ya kushambulia maeneo au raia kwa njia isiyo sawa." "Hili sio shambulio la usawa na la haki."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.