Pata taarifa kuu

Mahakama ya Juu ya Israeli inapitia sheria kuhusu masharti ya kutokuwa na uwezo wa Waziri Mkuu

Nchini Israeli, mzozo kati ya Mahakama ya Juu na mamlaka ya kisiasa unaendelea kuhusu mageuzi ya mfumo wa mahakama wenye utata. Mahakama ya juu zaidi nchini inatazamiwa kuchunguza sheria iliyopitishwa hivi majuzi na Bunge Jumanne hii. Hili ni andiko linaloweka ukomo wa masharti ya kutokuwa na uwezo wa Waziri Mkuu, yaani kesi ambazo atagetangazwa kuwa hafai kutekeleza majukumu yake.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Juni 25, 2023.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Juni 25, 2023. AP - Abir Sultan
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifah

Sheria hii, iliyopitishwa mwezi Machi mwaka huu kama sehemu ya mageuzi ya mfumo wa mahakama, ilifanywa na kambi ya Benjamin Netanyahu, kwa ajili ya Benjamin Netanyahu. Kufuatia sheria hiyo, ni Waziri Mkuu wa Israeli pekee anayeweza kujitangaza kuwa hafai kutekeleza majukumu yake, ikiwa atakuwa na matatizo ya kiafya au matatizo mengine.

Serikali pia inaweza kusababisha utaratibu huu wa kutokuwa na uwezo, lakini hii inahitaji kura ya robo tatu ya mawaziri. Inatosha kusema kwamba kutokana na sheria hii, Benjamin Netanyahu amejizatiti vilivyo.

Hata hivyo kutokana na kupitishwa kwa sheria hii msimu wa masika uliopita ambapo mkuu wa serikali ya Israel alienda kutetea kwa nguvu zote mageuzi yake ya mfumo wa mahakama. Kabla ya hapo, alijiweka kando. Kwa sababu "mikono yake ilikuwa imefungwa", alikiri hadharani.

Benjamin Netanyahu anashtakiwa katika kesi tatu za jinai. Kutaka kurekebisha mfumo wa mahakama ukiwa kizimbani ni wazi kunaleta mgongano wa kimaslahi. Naye Waziri Mkuu wa Israel alihofia kuondolewa madarakani wakati huo. Kutokana na sheria hii, alihakikisha aina ya kinga. Mahakimu wa mahakama ya juu zaidi nchini wanakutana Jumanne hii kusema iwapo sheria hii ni halali au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.