Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Israel yapanga kufungua ubalozi mjini Kinshasa na DRC kuhamisha wake Jerusalem

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Waziri Mkuu wa Israel wamefanya mkutano na waandishi wa habari kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2023. Waziri Mkuu wa Israel imetangaza kufungua ubalozi wake jijini Kinshasa na rais wa DRC kutangaza kuhamisha ubalozi wa DRC kutoka Tel Aviv kwebda Jerusalem. Ishara mpya ya kudumosha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Maelezo.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. © Photos Reuters & AFP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Waziri Mkuu wa Israel wameamua kuboresha zaidi uhusiano kati ya nchi zao mbili.

Kando ya vikao vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Benjamin Netanyahu ametangaza ufunguzi ujao wa ubalozi wa Israel mjini Kinshasa.

Kwa upande wake, Félix Tshisekedi ameelezea dhamira yake ya kuhamisha ubalozi wa Kongo kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem mara tu uamuzi wa mwenzake wa Israel utakapotekelezwa.

Uhusiano ambao pia utajumuisha uwekezaji katika maeneo mbalimbali

Waziri Mkuu wa Israel ametaja mazungumzo yake na rais Felix Tshisekedi kuwa yalizaa matunda, wakati rais Tshisekedi akiyataja kuwa mazuri.

Mazungumzo haya, ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa, yalifanya kupatikane kwa makubaliano, ambayo pande zote mbili zinaelezea kuwa ya manufaa.

Makubaliano hayo pia yatahusisha uwekezaji katika maeneo mbalimbali, yakiwemo ya usalama, yakilenga zaidi masuala ya usalama wa mtandao, kilimo na miundombinu.

Hadi wakati huo, mwanadiplomasia wa Israel anayehusika na uhusiano na DRC ana makaazi yake huko Luanda, nchini Angola.

Ilikuwa mwezi Novemba mwaka jana ambapo Shimon Solomon, mbunge wa zamani wa bunge la Israel, aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Félix Tshisekedi.

Nia ya mara kwa mara ya Félix Tshisekedi kwa Israel

Kwa upande wake rais wa DRC amekuwa akionyesha nia yake kwa Israel tangu aingie madarakani.

Aliongeza idadi ya mikutano isiyo rasmi na mikutano rasmi na wawakilishi wa kidini na maafisa wa Israeli.

Mnamo mwaka 2020, aliunga mkono hata mpango wa amani wa rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ambao ulikosolewa kwa madai ya athari mbaya kwa Palestina.

Wakati huo, rais Tshisekedi pia meelezea nia yake ya kuanzisha sehemu ya kiuchumi ya ubalozi wa Kongo mjini Jerusalem, kuashiria kuondoka kwake kwenye msimamo rasmi wa Umoja wa Afrika.

Kwa upande wake, Israel inaiona DRC kama mshirika anayewezekana kupata hadhi ya mashauriano katika Umoja wa Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.