Pata taarifa kuu

Israel:Mahakama ya juu kusikiliza kesi kuhusu mabadiliko ya sheria

Nairobi – Mahakama ya Juu ya Israel imeanza kusikiliza kesi inayolenga kupinga  kipengele kikuu cha marekebisho ya sheria yenye utata ya serikali ya mrengo wa kulia ambayo yamesababisha maandamano makubwa na kuligawa taifa hilo.

Majaji wote 15 wa Mahakama ya Juu ya Israel wamefika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kuangalia uhalali wa sheria iliyopitishwa na  wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu .
Majaji wote 15 wa Mahakama ya Juu ya Israel wamefika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kuangalia uhalali wa sheria iliyopitishwa na wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu . AP - Debbie Hill
Matangazo ya kibiashara

Jopo la majaji 15 wa mahakama ya juu limekutana kusikiliza maombi ya kupinga kubadilishwa kwa kile kinachoitwa kifungu cha busara ambacho serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilipitisha bungeni mwezi Julai.

Serikali yake waziri wa sasa Benjamin Netanyahu ilipitisha marekebisho ya katiba kwa kura 64 bila ya upinzani kwenye bunge la Israeli.

Haya yanajiri wakati huu maandamano yakidumu kwa zaidi ya miezi tisa tangu kuanza kwa mchakato huo januari mwaka huu.

Marekebisho hayo yanayopendekezwa  yanaweka ukomo wa mamlaka ya mahakama ya juu kupitia upya na wakati mwingine kubatilisha maamuzi ya serikali, ambayo wapinzani wanasema yanafungua njia kwa utawala wa kimabavu.

Tangu kuzinduliwa kwa mipango hiyo ya serikali Januari mwaka huuu ,makumi kwa maelfu ya wapinzani wameandamana katika miji yote kutaka sheria hiyo kutupiliwa mbali.

Usiku wa kuamkia leo raia wameandamana huku wakiimba democrasia.

"Marekebisho ya sheria ya kimsingi ambayo yatajadiliwa mahakamani leo sio sheria ya msingi, ni hati isiyowajibika," kiongozi wa upinzani Yair Lapid alisema kwenye mtandao wake wa Facebook.

Utawala wa Netanyahu, muungano kati ya chama chake cha Likud na washirika wa Kiyahudi wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia na wa Orthodox, unasema kuwa mabadiliko ya kisheria yanahitajika ili kusawazisha mamlaka kati ya wanasiasa na mahakama.

Waziri wa Sheria Yariv Levin, msanifu mkuu wa mageuzi hayo, alisema kusikilizwa kwa kesi ya Jumanne ni pigo mbaya kwa demokrasia, kwani kwa mara ya kwanza mahakama ilikuwa inafikiria kutupilia mbali sheria ya msingi, sheria ambayo nchini Israeli inachukua nafasi ya katiba.

"Mahakama, ambayo majaji wake hujichagua wenyewe kwa siri na bila rekodi, inajiweka juu ya serikali, bunge, wananchi na sheria," alisema katika taarifa yake.

"Hii ni kinyume kabisa na demokrasia. Ina maana kwamba mahakama haina cheki na mizani. Ni mtawala mmoja."

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti baadhi ya hatua kuelekea maelewano kati ya serikali na upinzani.

Israel haina katiba au baraza la juu la bunge, na sheria iliwekwa ili kuruhusu majaji kuamua ikiwa serikali ilivuka mamlaka yake.

Mahakama ya Juu ilitumia hatua hiyo katika uamuzi wa hali ya juu ambao ulimzuia Aryeh Deri, mshirika wa Netanyahu, kuhudumu katika baraza la mawaziri kwa sababu ya hatia ya kukwepa kulipa kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.