Pata taarifa kuu

Iran yamuachia Olivier Vandecasteele katika kubadilishana wafungwa

Raia huyo wa Ubelgiji alikuwa amezuiliwa nchini Iran kwa siku 455. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, mwanadiplomasia Assadollah Assadi, aliyehukumiwa nchini Ubelgiji kifungo cha maisha kwa kujaribu kupanga shambulio dhidi ya mkusanyiko wa Mujahedin wa raia huko Paris, pia ameachiliwa huru.

Maandamano ya kumuunga mkono raia wa Ubelgiji Olivier Vandecasteele aliyejihusisha na masuala ya kutoa misaada ya kibinadamu mjini Tournai, Ubelgiji tarehe 22 Aprili 2022.
Maandamano ya kumuunga mkono raia wa Ubelgiji Olivier Vandecasteele aliyejihusisha na masuala ya kutoa misaada ya kibinadamu mjini Tournai, Ubelgiji tarehe 22 Aprili 2022. AFP - JUSTIN NAMUR
Matangazo ya kibiashara

Raia huyu wa Ubelgiji Olivier Vandecasteele, aliyezuiliwa nchini Iran kwa siku 455, aliachiliwa baada ya kubadilishana wafungwa kati ya Brussels na Tehran iliyowezeshwa na Oman, maafisa kadhaa wakuu wametangaza Ijumaa.

"Olivier amekaa gerezani kwa siku 455 huko Tehran. Katika mazingira yasiyovumilika. Mtu ambaye hakuwa na hatia. Ikiwa yote yataenda kama ilivyopangwa, atakuwa nasi usiku wa leo. Hatimaye atakuwa huru,” Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo amesema, bila kurejelea mabadilishano ya wafungwa. Kwa upande wake, mamlaka ya Oman, mpatanishi kati ya Tehran na nchi za Magharibi, imebaini kwamba raia huyu wa Ubelgiji ameachiliwa kama sehemu ya "mabadilishano ya pamoja" ya wafungwa wawili kati ya Iran na Ubelgiji.

Wafungwa wawili wa zamani "walisafirishwa kutoka Tehran na Brussels hadi Muscat leo (Ijumaa) kwa nia ya kurejea katika nchi zao", mamlaka ya Oman imesema, bila kutoa maelezo juu ya utambulisho wa raia huyu wa Iran.

Mazungumzo na mwanadiplomasia wa Iran

Mwishoni mwa Aprili, Ubelgiji ilionyesha kuwa "inachunguza" ombi la Tehran la kuhamishwa kwa mwanadiplomasia wa Irani, Assadollah Assadi, aliyehukumiwa huko Antwerp mnamo 2021 hadi miaka ishirini jela kwa shambulio lililopangwa ambalo lililenga mkutano wa Kitaifa. Baraza la Upinzani wa Irani (NCRI, muungano wa wapinzani) mnamo 2018 huko Ufaransa. Mkataba wa uhamisho wa wafungwa uliotiwa saini mwaka 2022 kati ya Ubelgiji na Iran na ambao ulianza kutekelezwa tarehe 18 Aprili ulifungua njia ya mabadilishano haya.

Makumi ya Wamagharibi wanazuiliwa nchini Iran, wakielezewa na wanaowaunga mkono kama watu wasio na hatia wanaotumiwa na Tehran kama njia ya kujiinua na kujadiliana.

Olivier Vandecasteele, 42, ambaye alilikamatwa mnamo Februari 24, 2022 huko Tehran,  alipatikana na hatia ya "ujasusi". 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.