Pata taarifa kuu

Taliban wamuua gaidi aliyepanga shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul

NAIROBI – Kundi la Taliban limemuua gaidi wa Islamic State ambaye alipanga njama ya shambulio baya katika uwanja wa ndege wa Kabul wakati wa uhamishaji wa ghasia nchini Afghanistan mnamo 2021.

Shambulio hilo la mwaka 2021 lilijeruhi zaidi ya watu 170 na wanajeshi 13 wa Marekani
Shambulio hilo la mwaka 2021 lilijeruhi zaidi ya watu 170 na wanajeshi 13 wa Marekani AP - Lance Cpl. Nicholas Guevara
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la mwaka 2021 lilijeruhi zaidi ya watu 170 na wanajeshi 13 wa Amerika

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliwaua Waafghanistan waliokuwa wamekusanyika karibu na moja ya lango la kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai na wanajeshi wa Marekani wakiwachunguza.

Shambulio la Agosti 26 lilikuwa mojawapo ya shambulizi mbaya zaidi za uondoaji wa machafuko wa wanajeshi wa Marekani na wanadiplomasia baada ya miaka 20 ya vita nchini Afghanistan.

Afisa huyo wa Marekani, ambaye hakuruhusiwa kuzungumza hadharani, aliithibitishia kwamba Taliban walimuua mpangaji mkuu wa shambulio hilo.

Wanajeshi 11 raia wa marekani na mabaharia 11 waliuawa katika shambulio hilo. Mlipuko huo ulijeruhi wanajeshi 45 zaidi wa Marekani, wakiwemo baadhi waliopata majeraha mabaya ya ubongo.

Kiongozi huyo wa IS aliuawa wiki kadhaa zilizopita, lakini ilichukua muda kuthibitisha kifo chake, maafisa wa Marekani wamethibitisha japokuwa jina lake bado halijatangazwa.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa walikuwa wametambua kupitia ujasusi wao na ufuatiliajiwa kanda kwamba kiongozi huyo amefariki , ingawa hawakutoa maelezo zaidi kuhusu ni vipi walifahamu kuwa alikuwa ndiye muhusika wa mashambulio ya mabomu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.