Pata taarifa kuu

Mkuu wa diplomasia ya Saudia kuzuru Damascus

Mkuu wa diplomasia ya Saudia Faisal ben Farhane anatarajiwa, Jumanne Aprili 18, huko Damascus, nchini Syria, kwa ziara ya kwanza ya afisa wa Saudi arabia tangu mwanzo wa vita mwaka 2011, imetangaza wizara ya Habari ya Syria, shirika la habari la AFP limeripoti.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhane hapa alikuwa Misri mnamo Septemba 6, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwanamfalme Faisal bin Farhane hapa alikuwa Misri mnamo Septemba 6, 2022. AP - Amr Nabil
Matangazo ya kibiashara

Waandishi wa habari wamealikwa na Wizara ya Habari ya Syria kusafiri hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus ili kuripoti ujio wa Waziri wa Saudi Arabia Faisal bin Farhane, uliopangwa kufanyika mchana.

Mahusiano yalivunjika tangu 2012

Ziara yake inakuja wiki moja baada ya ile ya mwenzake wa Syria Faisal Moqdad nchini Saudi Arabia, ambayo pia ni ya kwanza tangu kuanza kwa vita. Damascus ilikuwa imetengwa kidiplomasia tangu mwaka wa 2011 kufuatia kukandamizwa kwa maandamano ya kiraia na kusababisha mzozo.

Saudi Arabia, kiongozi wa nchi za Ghuba, ilikata uhusiano na Damascus mwaka 2012 na hata kuwaunga mkono waasi mwanzoni mwa vita, katika nchi ambayo imekuwa uwanja wa vita kati ya vikosi vya kigeni. Lakini baada ya tetemeko la ardhi la Februari lililotikisa Uturuki na Syria, ufalme huo ulifanya ishara ya kwanza kwa kutuma msaada wa kibinadamu.

Mwezi Machi, Syria na Saudi Arabia walikuwa na majadiliano juu ya kurejea kwa huduma zao za kibalozi na Aprili 12, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria alifanya ziara ya kushtukiza huko Jeddah (magharibi mwa ufalme huo). Katika taarifa yao ya pamoja, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Syria na Saudi walitaja lengo la "kuirejesha Syria katika kundi la nchi za Kiarabu".

Rais wa Syria Bashar al-Assad alisema katika mahojiano mwezi uliopita kwamba Saudi Arabia "imechukua mkondo tofauti katika miaka ya hivi karibuni", na kwamba Syria sio "uwanja wa vita kati ya Saudi Arabia na Iran". Maridhiano ya Syria na Saudia yanakuja katika hali ambayo mvutano umepunguwa kati ya Saudi Arabia na mpinzani wake mkuu wa kikanda, Iran, ambayo inaunga mkono utawala wa Damascus kisiasa, kijeshi na kiuchumi.

Viongozi hao wawili wakubwa katika Mashariki ya Kati, ambao walivunja uhusiano wao mwaka 2016, walikuwa wamehitimisha mwezi Machi makubaliano ambayo hayakutarajiwa, yaliyosimamiwa na China, kwa nia ya kurejesha uhusiano wao. Nchi hizo mbili ziliahidi kufanya kazi pamoja kwa ajili ya "usalama na utulivu wa kanda nzima".

Kufadhili ujenzi wa Syria

Bashar naomba nchi hii tajiri ya Ghuba ili kufadhili ujenzi wa miundombinu ya nchi yake iliyoharibiwa na vita. Mzozo huo uligharimu maisha ya watu takriban nusu milioni. Karibu nusu ya Wasyria sasa ni wakimbizi au wakimbizi wa ndani, na maeneo mengi ya nchi hiyo bado yanaepuka udhibiti wa serikali. Lakini suala la kurudi kwa Syria kwenye kundi la nchi za Kiarabu si la kauli moja, hasa miongoni mwa wafalme wa Ghuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.