Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Saudi Arabia kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Iran na Syria

Saudi Arabia ilipokea Jumatano hii, Aprili 12, ujumbe wa Iran, ambao ulikuja kufungua tena ujumbe wa kidiplomasia katika ufalme huo, pamoja na mkuu wa diplomasia ya Syria, kama sehemu ya kurejesha uhusiano wa kiiplomasia uliokuwa ulivunjikwa kwa miaka kadhaa kwa nchi hizi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Faisal Meqdad akiwa na Walid al-Khuraiji mjini Jeddah Aprili 12, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Faisal Meqdad akiwa na Walid al-Khuraiji mjini Jeddah Aprili 12, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya wajumbe wa Iran imekuja siku chache baada ya mkutano wa kihistoria mjini Beijing wa wakuu wa diplomasia wa nchi hizo mbili, ambazo zilikata uhusiano wao mwaka 2016. Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal Meqdad, inakuja kabla ya kufanyika siku ya Ijumaa Aprili 14 huko Saudi Arabia mkutano wa nchi tisa za Kiarabu kuangazia kurejeshwa kwa Syria kwenye Jumuiya ya Waarabu, wakati mkutano ujao wa kawaida wa viongozi wa Kiarabu umepangwa kufanyika Mei 19 nchini Saudi arabia.

Damascus ilitengwa kidiplomasia tangu ukandamizaji wa mwaka 2011 wa uasi wa wananchi ambao ulizusha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo viliongezeka zaidi kwa miaka mingi baada ya nchi kadhaa na makundi ya kigeni yenye silaha kungila kati. Lakini nchi nyingi zaidi za Kiarabu sasa zinaunga mkono kurejeshwa kwa Syria kaika Jumuiya ya Waarabu. "Ujumbe wa Iran na ule wa Syria wako nchini Saudi Arabia siku moja. 

Hivi karibuni Riyadh na Tehran zilihitimisha makubaliano, yaliyosimamiwa na China, kwa ajili ya kurejesha uhusiano wao na watafungua tena balozi zao katikati ya mwezi Mei na kutekeleza makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na usalama yaliyosainiwa zaidi ya miaka ishirini. "Kwa mujibu wa makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia juu ya kuanza tena shughuli za kidiplomasia (...), ujumbe wa kiufundi wa Iran uliwasili Riyadh siku ya Jumatano na kupokelerwa na maafisa wa Saudi",  alitangaza msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kanani. "Ujumbe wa Iran utachukua hatua zinazohitajika kuunda ubalozi na uwakilishi mdogo huko Riyadh na Jeddah, pamoja na shughuli ya mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu", ameongeza Nasser Kanani.

Rais wa Iran kufanya ziara nchini Saudi Arabia mwishoni mwa mwezi Aprili

Riyadh na Tehran, vigogo wawili katika Mashariki ya Kati, walikuwa wamekatisha uhusiano wao baada ya shambulio la balozi za Saudia nchini Iran na waandamanaji waliolaani kunyongwa kwa mhubiri mashuhuri wa Kishia huko Saudi Arabia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.