Pata taarifa kuu

Iran: Polisi yachukua hatua kulazimisha uvaaji wa vazi la Kiislamu

Polisi ya Iran ilitangaza kuanza kutumika kwa hatua mpya za kudhibiti uvaaji wa hijab kuanzia Jumamosi Aprili 15 na kuwalazimisha wanawake kuheshimu uvaaji wa hijabu nchini Iran tangu mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979. Jumapili hii, polisi wamepitisha hatua kutekeleza uvaaji wa sitara ya Kiislamu.

Wanawake wa Iran wakitembea barabarani Aprili 15, 2023, huku mamlaka ikitangaza utekelezaji wa hatua mpya ya uvaaji hijabu huko Tehran.
Wanawake wa Iran wakitembea barabarani Aprili 15, 2023, huku mamlaka ikitangaza utekelezaji wa hatua mpya ya uvaaji hijabu huko Tehran. via REUTERS - WANA NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi

Kulingana na msemaji wa polisi, jumbe 3,500 za onyo zilitumwa kwa mikahawa, migahawa au vituo vya ununuzi kwa kutoheshimu uvaaji wa hijabu na 137 kati yazo zilifungwa kote nchini kwa kurudia kosa hilo.

Polisi ilitangaza kwamba kamera mpya za uchunguzi zitafanya iwezekane kutambua kwenye barabara, kwenye magari au katika vituo vya ununuzi, wanawake ambao hawaheshimu uvaaji wa hijabu.

Maonyo ya SMS pia yalitumwa kwa wanawake ambao hawavai sitara ya Kiislamu na, ikitokea kurudi kosa, watafikishwa mbele ya mahakama. Watalazimika kulipa faini na watanyimwa baadhi ya huduma za kijamii na wanaweza kuzuiwa kuondoka nchini. Magari yanayoendeshwa na wanawake ambao hawajavaa hijabu yanaweza kukamatwa kwa wiki kadhaa.

Tangu kifo cha Mahsa Amini mwezi Septemba, aliyekamatwa na polisi wa maadili kwa kutoheshimu uvaaji wa hijabu, idadi ya wanawake wasiovaa hijabu mitaani imeongezeka kama ishara ya kupinga.

Hatimaye naibu mwendesha mashtaka nchini humo ametangaza kuwa wale wanaowahimiza wanawake kutovaa hijabu wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka kumi jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.