Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-USALAMA

Iran ilitumia ndege za misaada ya tetemeko la ardhi kupeleka silaha Syria

Shirika la habari la Reuters limefichua kuwa Iran imetuma zana za kijeshi zilizofichwa kama nyenzo za misaada kwa Syria, kama sehemu ya misaada ya kibinadamu kwa manusura wa tetemeko baya la ardhi la Februari 6. Israel ilijibu kwa kufanya mashambulizi yaliyolenga uwanja wa ndege wa Aleppo, kulingana na uchunguzi huu.

Baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6 ambalo lilipiga kaskazini mwa Syria na Uturuki, mamia ya ndege kutoka Iran zilitua katika viwanja vya ndege vya Aleppo, Damascus na Latakia zikileta vifaa kwa kipndi cha wiki saba, vyanzo vimesema.
Baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6 ambalo lilipiga kaskazini mwa Syria na Uturuki, mamia ya ndege kutoka Iran zilitua katika viwanja vya ndege vya Aleppo, Damascus na Latakia zikileta vifaa kwa kipndi cha wiki saba, vyanzo vimesema. AFP - LOUAI BESHARA
Matangazo ya kibiashara

Betri za rada, vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano, vipuri vya mfumo wa ulinzi wa anga... Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la Reuters, ambalo linajikita kwa vyanzo tisa vya asili ya Syria, Iran, Israel na Magharibi, Iran imenufaika na ndege ya kusafirisha misaada ya kibinadamu kwenda Syria, kufuatia tetemeko la ardhi ya Februari 6, kupeleka silaha na vifaa vya kijeshi kwa mshirika wake.

Kwa mujibu wa vyanzo hivi, lengo lilikuwa kuimarisha ulinzi wa Iran dhidi ya Israel nchini Syria na kuimarisha nafasi ya Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Baada ya tetemeko la ardhi la Februari 6 ambalo lilipiga kaskazini mwa Syria na Uturuki, mamia ya ndege kutoka Iran zilitua katika viwanja vya ndege vya Aleppo, Damascus na Latakia zikileta vifaa kwa kipndi cha wiki saba, vyanzo vimesema.

Vifaa hivyo vilijumuisha vifaa vya hali ya juu vya mawasiliano, betri za rada na vipuri vinavyohitajika kwa ajili ya kuboresha mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria uliopangwa kuwa wa kisasa unaotolewa na Iran kama sehemu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vimesema vyanzo viwili vya kikanda na afisa mmoja kutoka moja ya nchi za Magharibi.

(Pamoja na Reuters)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.