Pata taarifa kuu
URUSI-ISRAEL-IRAN-EU

Urusi: Lazima nchi ya Iran ijumuishwe kwenye mazungumzo ya amani nchini Syria

Nchi ya Urusi imesema ni lazima Serikali ya Iran ihusishwe kwenye mazungumzo ya kusaka aamani ya Syria kama kiungo muhimu na mshirika wa karibu wa utawala wa rais Bashar al-Assad.Kauli ya Urusi inamaanisha kupuuzilia mbali maombi ya baadhi ya mataifa ya magharibi ambayo yametaka kujumuishwa kwenye mkutano wa kimataifa wa mjini Geneva, mkutano unaolenga kusaka amani ya kudumu nchini Syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiteta na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiteta na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia) Reuters
Matangazo ya kibiashara

Lakini kauli ya sasa ya Urusi kutaka nchi ya Iran nayo iingie kwenye mazungumzo ya kusaidia kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Syria imekosolewa na nchi za magharibi ambazo zinaiona Iran kama mfadhili mkuu wa silaha kwa wapiganaji wa Hezbollah wanaousaidia utawala wa Assad.

Hapo jana waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesisitiza nchi yake kutuma silaha zaidi za kijeshi kwa utawala wa Syria, silaha ambazo ni maalumu kwaajili ya kulinda anga la nchi hiyo.

Mpango huo wa Syria tayari umeibusha mgawanyiko kati yake na washirika wanaotaka amani nchini Syria ambapo wamekosoa hatua hiyo wakisema inalenga kuuimarisha utawala wa rais Assad.

Nchi ya kwanza kulaani kitendo hicho cha Urusi ni taifa la Israel ambalo lenyewe wazi limesema oitachukua hatua inazojua yenyewe iwapo mitambo hiyo maalumu itapelekwa nchini Syria, kitisho ambacho kinafungua ukurasa mwingine wa vita vya Syria.

Hatua ya Urusi inakuja ikiwa zimepita saa chache toka viongozi wa Umoja wa Ulaya wakubaliane kuwaondolea vikwazo vya silaha waasi wa Syria japokuwa hakuna nchi iliyotangaza wazi ni lini itaanza kupeleka silaha kwa waasi hao.

Marekani licha ya kuunga mkono hatua ya Umoja wa Ulaya bado imeendelea kuonesha wasiwasi wake kuhusu silaha hizo kufika kwenye mikono ya makundi ya kigaidi ambayo yanatishia usalama wa mataifa ya magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.