Pata taarifa kuu

Iran: Visa vipya vya wasichana wa shule kupewa sumu vyaorodheshwa

Makumi ya wasichana wadogo wamepewa sumu Jumamosi hii katika shule kadhaa kote Iran, nchi iliyotikiswa kwa zaidi ya miezi minne na visa vya ajabu wasichana wa shule kupewa sumu, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Visa hivi vilianza miezi miwili baada ya kuanza kwa maandamano nchini Iran kupinga kifo cha Mahsa Amini (Septemba 16), msichana aliyezuiliwa na polisi wa maadili ambao walimtuhumu kwa kuvunja sheria kali ya mavazi  ya hijabu iliyowekwa hasa kwa wanawake.
Visa hivi vilianza miezi miwili baada ya kuanza kwa maandamano nchini Iran kupinga kifo cha Mahsa Amini (Septemba 16), msichana aliyezuiliwa na polisi wa maadili ambao walimtuhumu kwa kuvunja sheria kali ya mavazi ya hijabu iliyowekwa hasa kwa wanawake. ROSLAN RAHMAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwishoni mwa mwezi Novemba, shule nyingi wanakosomea wasichana, zimeathiriwa na sumu inayosababishwa na gesi au vitu vya sumu, na kusababisha wasichana kuzirai au kupoteza fahamu, wakati mwingine wakilazwa hospitalini.

Akinukuliwa na runinga ya taifa siku ya Ijumaa, mkuu wa Tume ya Kitaifa ya Kutafuta Ukweli katika kesi hii, Mbunge Hamidreza Kazemi, amesema kuwa ripoti ya mwisho ya tum hiyo itachapishwa 'baada ya wiki mbili'.

Shida ya kupumua na maumivu ya kichwa

Angalau "wanafunzi 60 wamepewa sumu (Jumamosi hii) katika shule ya wasichana huko Haftkel", katika jimbo la Khuzestan, shirika la habari la Iribnews limesema, likimnukuu afisa wa eneo hilo.

Wasichana wa shule pia wamepewa sumu katika "shule tano huko Ardabil, kaskazini-magharibi", ambapo waliwasilisha "dalili za wasiwasi, upungufu wa pumzi na maumivu ya kichwa", kimeongeza chanzo kimoja.

Katika Urmia, mji mkuu wa jimbo la Azabajani Magharibi, "idadi isiyojulikana" ya wanafunzi kutoka shule ya msingi pia wameathirika "baada ya kushuku kuwa wamepewa sumu", limebaini kwa upande wake shirika la habari la Ilna, bila maelezo zaidi.

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alitoa wito Machi 6 kwa "adhabu kali", hadi kufikia adhabu ya kifo, dhidi ya wale ambao watapatikana na hatia ya visa hivi.

Visa hivi vilianza miezi miwili baada ya kuanza kwa maandamano nchini Iran kupinga kifo cha Mahsa Amini (Septemba 16), msichana aliyezuiliwa na polisi wa maadili ambao walimtuhumu kwa kuvunja sheria kali ya mavazi  ya hijabu iliyowekwa hasa kwa wanawake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.