Pata taarifa kuu

Iran: Kesi mpya ya kupewa sumu wanafunzi yaripotiwa katika shule ya wasichana

Wiki tatu baada ya kesi ya kesi ya kupewa sumu wanafunzi nchini Iran, kesi nyingine imeripotiwa katika shule ya wasichana nchini humo leo Jumanne, siku moja baada ya kuanza tena masomo baada ya wiki mbili za likizo, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Wasichana wadogo waliopewa sumu shuleni nchini Iran.
Wasichana wadogo waliopewa sumu shuleni nchini Iran. © Tasnim
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi ishirini wa shule moja ya Jiji la Tabriz (Kaskazini Magharibi) wamepelekwa hospitalini kwa shida za kupumua, shirika la serikali la IRNA limeripoti.

"Idara ya huduma za dharura imetuma kikosi chake eneo la tukio baada ya wanafunzi kadhaa 'kupata usumbufu wa kupumua, amesema mkuu wa Idara ya huduma za dharura'.

Lakini, amebaini kwamba, "hakuna hata mmoja wao ambaye alikuwa katika hali mbaya. "

Tangu mwisho wa mwezi Novemba, shule nyingi, hasa za wasichana, zimeathiriwa na sumu na gesi au vitu vyenye sumu ambavyo vimesababisha usumbufu na kusababisha kutapika wakati mwingine kulazwa hospitalini.

'Zaidi ya wanafunzi 5,000' wameathiriwa tangu mwisho mwa mwezi Novemba

Kwa jumla, viongozi wameorodhesha 'zaidi ya wanafunzi 5,000' katika shule zaidi ya 230 katika mikoa 25 kati ya 31. Matukio haya yalisitishwa baada ya viongozi kutangaza mapema mwezi Machi kuwakamata mamia ya washukiwa wa vitendo hivyo viovu.

Siku chache mapema, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, alitangaza 'adhabu kali', hadi adhabu ya kifo, dhidi ya watu ambao watatambuliwa kuwajibika kwa sumu hizi, akilaani 'uhalifu usiosameheka'.

Kutokana na ongezeko la visa hivi, wazazi wa wanafunzi na wakaazi walielezea wasiwasi wao na kuwaomba viongozi kuchukua hatua.

Kesi hiyo ilianza miezi miwili baada ya kuanza kwa maandamano yaliyozinduliwa nchini Iran kufuatia kifo cha Mahsa Amini, mwanamke aliyezuiliwa na polisi inayohusika na kushimisha mavazi ya dini mnamo Septemba 16 ambayo ilimtuhumu kwa kukiuka kanuni kali za mavazi zilizowekwa hasa kwa wanawake Kuvaa hijabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.