Pata taarifa kuu
MAGEUZI-MAHAKAMA

Israel: Pendekezo la maelewano la Isaac Herzog kuhusu mageuzi ya mahakama yafutiliwa mbali

Nchini Israeli, mageuzi ya mahakama yanayotafutwa na serikali yanaendelea kugawanya nchi. Katika wiki za hivi karibuni, rais wa Israel amezidisha wito wa mazungumzo kati ya serikali na upinzani. Mnamo Machi 15, Isaac Herzog aliwasilisha rasimu ya maelewano, lakini mara moja ilipingwa na serikali.

Mnamo Machi 15, Rais wa Israel Isaac Hertzog aliwasilisha rasimu ya maelewano kuhusu mageuzi ya mahakama ambayo yalikataliwa mara moja na serikali.
Mnamo Machi 15, Rais wa Israel Isaac Hertzog aliwasilisha rasimu ya maelewano kuhusu mageuzi ya mahakama ambayo yalikataliwa mara moja na serikali. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa

Nchini Israeli, jukumu la rais ni la kusindikiza tu. Bila nguvu halisi, Isaac Herzog anajitahidi licha ya kila kitu, kujaribu kukomesha mgogoro huu, unaosababishwa na mageuzi ya vyombo vya sheria. Rais hukutana na viongozi kutoka walio wengi, kutoka upinzani, anazungumza na kambi zote mbili, na anajaribu kutoa suluhisho thabiti.

Jioni ya Machi 15, aliwasilisha maandishi yanayoitwa "Maelewano ya raia". Kwa undani, Isaac Herzog anapendekeza hasa mabadiliko katika hoja zenye utata za mageuzi yaliyotangazwa na serikali. Kwa maneno mengine, sheria hizi ambazo zitamruhusu Benjamin Netanyahu na washirika wake kuwa na nguvu zote, na kuangamiza uwezo wa Mahakama ya Juu.

Hali ni mbaya: “Yeyote anayefikiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe haviwezekani, hajui jinsi tulivyovikaribia. Lakini sitairuhusu vifanyike, "anaonya rais wa Israel. Anaeleza kwamba ana hakika kwamba "Waisraeli, kwa wingi wao, wanataka maelewano". Upinzani unakaribisha mpango huu. Serikali inakataa kabisa.

Mageuzi haya yenye utata, yanayotafutwa na serikali ya Benjamin Netanyahu, na muungano wake wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia yanasababisha maandamano makubwa ya wananchi. Maandamano sasa yanafanyika kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.