Pata taarifa kuu

Tetemeko la Ardhi: Damascus yaidhinisha utoaji wa misaada ya kimataifa kwa maeneo ya waasi

Serikali ya Syria imetangaza Ijumaa kukubali kufikishwa kwa msaada wa kimataifa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo iliyoathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi.

Nchini Lebanon, mshikamano umepangwa kutuma msaada kwa Wasyria, waathiriwa wa tetemeko la ardhi. Picha zilizochukuliwa karibu na mji Sidon, Lebanon, Februari 10, 2023.
Nchini Lebanon, mshikamano umepangwa kutuma msaada kwa Wasyria, waathiriwa wa tetemeko la ardhi. Picha zilizochukuliwa karibu na mji Sidon, Lebanon, Februari 10, 2023. REUTERS - AZIZ TAHER
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la serikali ya Syria Sana, serikali imetaja kwamba usambazaji wa misaada ya kibinadamu unapaswa "kusimamiwa na shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu ya Syria", kwa msaada wa UUmoja wa Mataifa.

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika nchi ya Syria inafikia 3,377, ikimaanisha kuwa jumla ya walioaga dunia imefikia karibu 23,000.

"WFP inaomba dola milioni 77 kutoa msaada wa mgao wa chakula na vyakula vya moto kwa jumla ya watu 874,000 walioathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria," shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Roma limesema.

Siku nne baada ya mkasa huo mbaya, miujiza bado inaonekana kwa baadhi ya watu kuokolewa wakiwa hai kutoka chini ya vifusi. Katika mji wa Antakya, msichana wa miaka 10 ameokolewa usiku wa leo akiwa hai. Katika jimbo la Hatay nchini Uturuki, watu 9 wamegundulika kuwa hai baada ya kukwama kwenye jengo kwa muda wote.

Hayo yanajiri wakati msaada wa kwanza wa Umoja wa Mataifa ulifanikiwa kuwasili siku ya Alhamisi katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Syria lakini matumaini ya kuwapata manusura zaidi yamefifia tangu zipite siku tatu ambazo wataalamu wanazingatia kama kipindi muhimu cha kuokoa maisha ya binadamu. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.