Afghanistan: Kampuni ya China yatia saini mkataba wa uchimbaji mafuta na Taliban
Mkataba wa kwanza wa kimataifa wa uchimbaji mafuta ulitiwa saini mjini Kabul siku ya Alhamisi tarehe 5 Januari. Hundi ya dola milioni 750 ambayo itaiwezesha Beijing kutafuta mafuta kaskazini mwa Afghanistan na ambayo inaupa utawala mpya wa Afghanistan uwekezaji wa kigeni na maonyesho ya kimataifa unaohitaji.
Imechapishwa:
Makubaliano hayo yanataka kampuni ya Xinjiang Asia ya Kati ya Petroli na Gesi (CAPEIC) kuchimba mafuta katika bonde la Amu Darya, kulingana na BBC.
Taliban wameshinda yote
Kwenye karatasi, Taliban wameshinda kila kitu. Tangu kudhibitiwa kwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, wamekuwa wakitafuta pesa. Mkataba huo unatoa mrahaba wa 15% unaolipwa kwa utawala wa Afghanistan kwa kipindi cha miaka ishirini na mitano. Walitaka miundombinu mipya. China imekubali kujenga kiwanda cha kwanza cha kusafisha mafuta nchini Afghanistan. Jambo ambalo pia litatoa ajira. Kulingana na mamlaka ya Taliban, watu 3,000 kutoka eneo hilo watahusishwa na mradi huu.
Utakuwa mkataba wa kwanza mkubwa wa uchimbaji wa nishati na kampuni ya kigeni tangu Taliban kuchukua udhibiti wa Afghanistan mnamo 2021.
Kujitosheleza
Kampuni ya kitaifa ya mafuta ya China, ambayo ilianza shughuli zake nchini Afghanistan mwaka 2012, haitaki kuacha sehemu yake ya soko. Na haijalishi nani anatawala. Uzuri wa mkataba huu, kwa mujibu wa balozi wa China aliyekuwepo wakati wa kutiwa saini, ni kuweka uchumi wa Afghanistan kwenye njia ya kujitosheleza.