Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-ULINZI

Saudi Arabia kuanza kutengeneza makombora ya masafa marefu kwa usaidizi wa China

Saudi Arabia imeanza kutengeneza makombora ya masafa marefu kwa msaada kutoka China. Haya ni kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Marekani CNN, kwa mujibu wa mashirika ya kijasusi ya Marekani yanafahamishwa kuhusu ushirikiano huu kati ya Beijing na Riyadh. Ushirikiano ambao unaweza kuwa na athari kubwa.

Saudi Arabia sasa inatengeneza makombora yake kwa msaada kutoka Beijing, kulingana na CNN.
Saudi Arabia sasa inatengeneza makombora yake kwa msaada kutoka Beijing, kulingana na CNN. REUTERS/Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia tayari ina makombora yamasafa marefu yaliyotengenezwa na China, lakini CNN inasema nchi hiyo sasa inatengeneza makombora yake kwa usaidizi kutoka Beijing. Idhaa ya Marekani huchapisha picha za satelaiti zilizopigwa Dawadmi, magharibi mwa Riyadh, ambapo kunapatikana kiwanda cha uzalishaji.

Habari hii, ikiwa itathibitishwa, kwa mara nyingine tena inaonyesha mbio za kumiliki silaha huko Mashariki ya Kati, ambapo nchi za kifalme za Ghuba zinatumia gharama kubwa kujitayarisha na kudai uhuru wao, wakati ambapo mshirika wao Marekani anaelekea kujiondoa.

Makombora yaliyotengenezwa na Saudia pia yangetatiza mazungumzo na Iran. Yanahusiana na nyuklia, lakini nchi za Magharibi na washirika wao katika eneo la mashariki ya Kati wanaamini kwamba mpango wa kutengeneza makombra ya masafa marefu wa Tehran unaleta tishio na pia unapaswa kua moja ya masuala muhimu katika mazungumzo ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.