Pata taarifa kuu
UTURUKI

Mafuriko Uturuki: Karibu Themanini wafariki dunia, arobaini hawajulikani waliko

Mafuriko ambayo yalikumba eneo la kaskazini mwa Uturuki wiki iliyopita yameua watu wasiopungua 77, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa hivi punde na mamlaka, ambayo inaendelea kutafuta makumi ya watu ambao hawajulikani waliko.

Kulingana na wataalam, majanga ya asili kama haya yanayofuatana katika nchi hii yanaweza kuwa yakitokea mara kwa mara na yenye uharibifu mkubwa kutokana na ongezeko la joto linalosababishwa na shughuli za binadamu.
Kulingana na wataalam, majanga ya asili kama haya yanayofuatana katika nchi hii yanaweza kuwa yakitokea mara kwa mara na yenye uharibifu mkubwa kutokana na ongezeko la joto linalosababishwa na shughuli za binadamu. AFP - YASIN AKGUL
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na idara ya serikali ya usimamizi wa majanga ya asili (Afad), watu 40 bado hawajapatikana baada ya mafuriko yaliyotokea kufuati mvua kubwa kunyesha Jumatano wiki iliyopita katika majimbo yaliyoko kwenye Bahari Nyeusi.

Katika wilaya ya Bozkurt, moja ya maeneo yalioathirika zaidi, maafisa wa ifara ya uokoaji walitafuta mwishoni mwa wiki chini ya vifusi vya makaazi ya watu yaliyoharibiwa na mafuriko.

Mafuriko baada ya moto mkubwa

Mafuriko haya, ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Uturuki kwa miongo kadhaa, yalitokea wakati nchi hiyo ilikuwa ikiondokana katika janga lingine la moto mkubwa ambao ulisababish vifo vya watu wanane na kuharibu maeneo ya watalii kusini mwa nchi.

Kulingana na wataalam, majanga ya asili kama haya yanayofuatana katika nchi hii yanaweza kuwa yakitokea mara kwa mara na yenye uharibifu mkubwa kutokana na ongezeko la joto linalosababishwa na shughuli za binadamu.

Wanasiasa kadhaa na wanaharakati wameongeza shinikizo kwa rais Recep Tayyip Erdogan kuchukua hatua kali ilikupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Uturuki ni moja ya nchi chache ambazo hazikuidhinisha mkataba wa tabia nchi wa Paris wa mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.