Pata taarifa kuu
UTURUKI

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Uturuki yaongezeka hadi 31

Watu thelathini na moja wamefarki dunia kufuatia mafuriko katika eneo la Bahari Nyeusi nchini Uturuki, na zaidi ya watu 1,700 wamehamishwa, idara ya Maafa na Usimamizi wa Dharura (AFAD) imesema Ijumaa.

Watalii wanasubiri kuhamishwa na boti kutoka eneo linaloendelea kuathiriwa na moto wa misitu unaotokea chini ya kilima kuelekea kando ya bahari huko Bodrum, Mugla, Uturuki mnamo Agosti 1, 2021.
Watalii wanasubiri kuhamishwa na boti kutoka eneo linaloendelea kuathiriwa na moto wa misitu unaotokea chini ya kilima kuelekea kando ya bahari huko Bodrum, Mugla, Uturuki mnamo Agosti 1, 2021. AP - Emre Tazegul
Matangazo ya kibiashara

Hili ni janga la pili la asili kuikumba Uturuki mwezi huu baada ya moto mkubwa ulioathiri ukingo wa Mediterania.

Mafuriko hayo yamesababisha maafa katika majimbo ya kaskazini mwa nchi hiyo, wakati ambapo maafisa wamekuwa wakitangaza kuwa wameudhibiti moto wa misitu ambao umekuwa ukiwaka kwa wiki mbili katika maeneo ya kusini mwa pwani.

Watu ishirini na tisa wamefariki dunia katika mafuriko katika mkoa wa Kastamonu na wengine wawili wamefariki dunia huko Sinop, viongozi wamesema.

Zoezi la utafutaji linaendelea kujaribu kupata mtu aliyetoweka katika jimbo la Bartin.

AFAD inasema zaidi ya watu 1,700 wamehamishwa kutoka maeneo yaliyoathiriwa katika majimbo matatu, baadhi na helikopta na boti.

Pia kulingana na idara hiyo, mafuriko hayo yaliharibu miundombinu ya umeme, na zaidi ya vijiji 330 kukosa umeme. Madaraja matano yamedondoka na mengine mengi yameharibiwa, na kusababisha kufungwa kwa barabara kadhaa, AFAD imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.