Pata taarifa kuu
UTURUKI

Mafuriko nchini Uturuki: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 27

Takriban watu 27 wamefariki dunia katika mafuriko kaskazini mwa Uturuki, eneo ambalo limeathiriwa na majanga ya moto katika wiki za hivi karibuni, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa leo Ijumaa na mamlaka.

Uturuki imekuwa eneo la majanga kadhaa ya asili katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na vipindi vya ukame mkali na moto mkali wa misitu mwishoni mwa mwezi Julai na mapema mwezi Agosti.
Uturuki imekuwa eneo la majanga kadhaa ya asili katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na vipindi vya ukame mkali na moto mkali wa misitu mwishoni mwa mwezi Julai na mapema mwezi Agosti. AFP - YASIN AKGUL
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja bado hajapatikana wakati shughuli kubwa ya utaftaji na uokoaji inaendelea, viongozi wanaohusika na kusimamia majanga ya asili wamesema.

Ripoti rasmi ya hapo awali iliripoti vifo 17 siku moja kabla. Kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki, rais Recep Tayyip Erdogan anatarajia kuzuru mkoa mmoja ulioathirika zaidi leo Ijumaa kuona uharibifu na kutoa msaada kwa wahanga.

Mafuriko hayo, ambayo yaliathiri zaidi majimbo ya Kastamonu, Bartin na Sinop, yaliyoko ufukweni mwa Bahari Nyeusi, yalisababishwa na mvua kubwa usiku kucha kutoka Jumanne hadi Jumatano.

Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, kiwango cha maji kiliongezeka hadi mita nne katika baadhi ya miji, mamlaka imesema, na mitaa ya miji yote iligeuka mito iliyobeba magari na kila aina ya uchafu.

Wanasayansi wengi wanabaini kwamba hali hiyo ni kutokana na uhusiano kati ya ongezeko la joto ulimwenguni linalosababishwa na shughuli za binadamu na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa.

Uturuki imekuwa eneo la majanga kadhaa ya asili katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na vipindi vya ukame mkali na moto mkali wa misitu mwishoni mwa mwezi Julai na mapema mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.