Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Mazungumzo yaendelea kati ya serikali na Taliba

Wajumbe kutoka serikali ya Kabul na Taliban wanaokutana nchini Qatar kutafuta suluhu ya mzozo nchini Afghanistan wameahidi kuendelea na mazungumzo lakini swali la kusitisha mapigano halikuzungumzwa, Al Jazeera imeripoti, ikinukuu msemaji wa Taliban.

Ujumbe wa Taliban ukishiriki mazungumzo na serikali huko Doha, Qatar, Julai 17, 2021.
Ujumbe wa Taliban ukishiriki mazungumzo na serikali huko Doha, Qatar, Julai 17, 2021. KARIM JAAFAR AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na kituo cha habari cha Qatar, kambi hizo mbili zimeahidi katika taarifa ya pamoja "kuendelea na mazungumzo kwa kiwango cha juu hadi makubaliano yatakapofikiwa".

Wajumbe hao kutoka kambi hizo mbili wanaokutana tangu Jumamosi huko Doha pia wamekubali kuruhusu utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan,  kituo cha habari cha Al Jazeera kimeongeza.

Msemaji wa ofisi ya kuu ya kisiasa ya Taliban huko Qatar amekiambia kituo hicho kuwa suala la usitishaji mapigano halijawekwa mezani.

"Hatujawasilisha pendekezo la kusitisha mapigano kwa miezi mitatu wakati wa mazungumzo huko Doha," amesema, wakati waasi wa Kiislam wameendelea kusonga mbele katika wiki za hivi karibuni kote nchini baada ya vikosi vya mwisho vya wanajeshi wa Marekani kuanza kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.