Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban yadai kudbiti kituo kikuu cha mpakani na Pakistan

Taliban imetangaza Jumatano hii (Julai 14) kwamba wamechukuwa udhibiti wa kituo kikuu cha mpakani na Pakistan. Kwa hatua hii mpya, waasi wameitenga kabisa serikali ya Afghanistan kwa kupata nafasi ya kuvuka mpaka wa nchi hiyo na Pakistan kuchukua udhibiti kamili wa bidhaa zinazoingia Afghanistan. Habari inayopingwa na mamlaka ya Afghanistan, lakini imethibitishwa na nchi jirani ya Pakistan.

Msafara wa Vikosi Maalum vya Afghanistan katika mkoa wa Kandahar, Julai 13, 2021.
Msafara wa Vikosi Maalum vya Afghanistan katika mkoa wa Kandahar, Julai 13, 2021. REUTERS - DANISH SIDDIQUI
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku kadhaa, vituo muhimu vya mpakani vimeanguka moja kwa moja chini ya udhibiti wa Taliban. Baada ya kiile cha Shir Khan Bandar kaskazini mwa nchi, ambacho kiinadhibiti barabara ya kimkakati inayoelekea Tajikistan na Asia ya Kati, nyingine kwenye mpaka na Turkmenistan, na ile ya Islam Qala, kituo kikuu cha mpakani na Iran siku nne iliyopita, Taliban imetangaza kudhibiti Spin Boldak-Chaman, kituo kikuu cha mpakani kinahodhibiti barabara muhimu zaidi ya kibiashara kati ya Afghanistan na Pakistan.

Katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili ya mashambulizi makubwa, waasi wamefanikiwa kudhibiti mipaka ya nchi na kutoza ushuru wa forodha. Hili bado ni pigo jingine kwa vikosi vya Afghanistan ambavyo, baada ya kupoteza robo tatu ya nchi hiyo, sasa wanajikuta bila chanzo hiki muhimu cha kuingiza fedha.

Licha ya taarifa hii kukanushwa na maafisa wa Afghanistan ambao wanadai kuwa wamezima mashambulio ya waasi, video kadhaa zinathibitisha uwepo wa wapiganaji wa Taliban huko Spin Boldak, ambapo Taliban walipandisha bendera yao nyeupe ya dola la Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.