Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-USALAMA

Hatua ya Trump kuishambulia Iran yaishia hewani

Rais wa Marekani Donakd Trump alitaka kufanya mashambulizi dhidi ya kituo kikuu cha nyuklia nchini Iran wiki iliyopita, lakini mwishowe aliamua kutochukua hatua hiyo kali, amesema mwakilishi wa Marekani amebaini.

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw. Trump alitoa ombi hilo siku ya Alhamisi wakati wa mkutano na washauri wake wakuu wa usalama wa kitaifa, mkutano ambao pia walihudhuria Makamu wa rais Mike Pence, kaimu mkuu mpya wa Pentagon Christopher Miller, na Mkuu wa majeshi ya Marekanii, Jenerali Mark Milley, amesema mwakilishi huyo.

Donald Trump, ambaye anakataa kutambua ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais wa Novemba 3, anatarajia kukabidhi madaraka kwa Biden mnamo Januari 20.

Akiongea kwa sharti la kutotajwa jina, mwakilishi huyo amethibitisha ripoti ya Gazeti la New York Times kuhusu mkutano huo, ambayo inasema Donald Trump alishawishika na washauri wake kutofanya mshambulizi dhidi ya Iran kwa sababu ya hatari za mzozo kutokea kuwa mkubwa.

Sababu ya Trump kuulizia uwezekano huo wa kuishambulia Iran inatajwa kuwa ni ripoti ya Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) iliyosema kwamba Iran inaendelea na kukusanya madini ya uranium yanayotumika kutengenezea silaha za nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.