Pata taarifa kuu
IRAN-CORONA-AFYA

Coronavirus: Iran yavunja rekodi kwa maambukizi zaidi na vifo

Iran, nchi iliyoathiriwa vibaya zaidi na janga la Corona katika Mashariki ya Kati, imeripoti rekodi 13,053 za maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 486 vinavyotokana na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Siku ya Jumapili rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kwamba taifa na serikali vitaendelea na uhamasishaji wa jumla ili kukabiliana na wimbi la tatu la janga hilo, ambalo kusambaa kwake kumeongezeka kwa kasi ya kutisha katika wiki za hivi karibuni.
Siku ya Jumapili rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kwamba taifa na serikali vitaendelea na uhamasishaji wa jumla ili kukabiliana na wimbi la tatu la janga hilo, ambalo kusambaa kwake kumeongezeka kwa kasi ya kutisha katika wiki za hivi karibuni. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Iran imesema itaweka makataa mapya kuzuia kuenea kwa janga hilo.

Kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya, jumla ya idadi ya maambukizi imefikia sasa 775,121 na vifo 41,979.

Siku ya Jumapili rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kwamba taifa na serikali vitaendelea na uhamasishaji wa jumla ili kukabiliana na wimbi la tatu la janga hilo, ambalo kusambaa kwake kumeongezeka kwa kasi ya kutisha katika wiki za hivi karibuni.

Miongoni mwa vizuizi vikali zaidi ambavyo vitawekewa jijini Tehran na katika miji mingine 100 ya Iran kwa wiki mbili kuanzia Novemba 21, serikali ilitangaza Jumamosi kwamba imepanga kufunga biashara na huduma ambazo sio muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.