Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-AL QAEDA-USALAMA

Kiongozi wa Al-Qaeda Abu Muhsin al-Masri auawa Afghanistan

Vikosi maalum vya Afghanistan vimemuua kiongozi muhimu wa kundi la Al-Qaeda ambaye pia alikuwa akitafutwa na Marekani, idara ya ujasusi ya Afghanistan imesema.

Mwanajeshi wa jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Ghazni, Mei 18, 2020.
Mwanajeshi wa jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Ghazni, Mei 18, 2020. REUTERS/Mustafa Andaleb
Matangazo ya kibiashara

Abu Muhsin al-Masri, Mmisri aliyechukuliwa kama kiongozi nambari mbili wa kundi la Al-Qaeda mwenye ushawishi zaidi katika kundi hilo katika kanda hiyo ya India, aliuawa katika mkoa wa Ghazni katikati mwa Afghanistan, Idara ya kitaifa ya usalama nchini afghanista imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Idara hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya operesheni hiyo na hakuonyesha ni lini ilifanyika. Jina la Al-Masri liko kwenye orodha ya magaidi wanaotafutwa sana na shirika la upelelezi la FBI la Marekani.

Al-Masri alikuwa ameshitakiwa nchini Marekani kwa kutoa ufadhili wa bidhaa na raslimali kwa shirika moja la kigeni linalohusika na ugaidi na pia kwa njama ya kuwauwa raia wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.