Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Mazungumzo ya amani kufanyika nchini Qatar

Kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan wataanza mazungumzo ya moja kwa moja ya amani Jumamosi, Septemba 12 huko Doha, nchini Qatar.

Kuachiliwa huru kwa wafungwa 5,000 wa Taliban ilikuwa moja ya masharti ya kuanza mazungumzo ya amani. Hapa, wanamgambo wa Taliban wakiachiliwa huru Agosti 13, 2020 kutoka gereza la Pul-e-Charkhi huko Kabul.
Kuachiliwa huru kwa wafungwa 5,000 wa Taliban ilikuwa moja ya masharti ya kuanza mazungumzo ya amani. Hapa, wanamgambo wa Taliban wakiachiliwa huru Agosti 13, 2020 kutoka gereza la Pul-e-Charkhi huko Kabul. National Security Council of Afghanistan/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya, yaliyocheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita, yanatarajiwa kujaribu kumaliza karibu miaka 19 ya mgogoro kati ya pande hizo mbili hasimu nchini Afghanistan.

"Labda kujitokeze matatizo katika dakika za mwisho, timu ya (mazungumzo) ya serikali itaondoka kwenda Doha kesho, na tuna imani kuwa mazungumzo yatafanyika hivi karibuni, labda Jumamosi," chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habari la AFP. Ikulu ya rais nchini Afghanistan imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba ujumbe wake wa watu 21 utaondoka kwenda Doha leo Ijumaa.

Taliban wametangaza kuwa wako tayari kushiriki mazungumzo hayo. "Kuna uwezekano mkubwa kwamba mazungumzo yataanza Jumamosi," chanzo cha Taliban kimethibitisha katika taarifa, na kusisitiza juu ya nia yao ya "kuendeleza mchakato wa mazungumzo" na "kuleta amani kamili na mfumo safi wa Kiislam ndani ya mfumo wa maadili yao ya Kiislamu na masilahi yao ya kitaifa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.