Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-TALIBAN-USALAMA

Afghanistan: Serikali yaanza tena zoezi la kuachilia huru wanamgambo wa Taliban

Kufikia sasa, Kabul ilikuwa amewaachilia karibu wafungwa 5,000 lakini ilikataa kuwaachilia wafungwa 320 wanaoshtumiwa uhalifu mkubwa.

Wanamgambo wa Taliban waachiliwa huru Agosti 13 wakiondoka katika gereza la Pul-e-Charkhi huko Kabul.
Wanamgambo wa Taliban waachiliwa huru Agosti 13 wakiondoka katika gereza la Pul-e-Charkhi huko Kabul. National Security Council of Afghanistan/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili la kuawaachilia huru wanamgambo wa kundi la Taliban limekaribishwa na kundi hilo, na linaweza kufungua njia ya mazungumzo ya amani baian ya Waafghanistan.

Wanamgambo wa Taliban walikuwa wakisubiri mchakato huu kwa miaka mingi. Iliyotangazwa mwanzoni mwa Agosti, iliichukua karibu mwezi mmoja mamlaka nchini Afghanista kufungua milango ya jela ili kuwaachia mamia ya wanamgambo wa kundi hilo la Taliban.

Kuachiliwa kwao ni sehemu ya mpango mkubwa wa kubadilishana wafungwa. Kabul ilipinga mpango huo kwa muda mrefu. "Hakuna kuwategea sikio watu wasio wa kweli ambao wanataka tuwaachilia huru wafungwa walio hatari zaidi, ambao baadhi yao wameua raia wa kigeni, hasa raia wa Ufaransa, "awali ilitangaza serikali ya Kabul..

Lakini siku chache baadaye, serikali ya Afghanistan ilikubali masharti ya Taliban kwa sababu changamoto bado ni kubwa. Kabul inataka kugeuza ukurasa huo wa miaka kadhaa ya vita.

"Mpango huu ni hatua nzuri ya inayofungua njia ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Waafghanistan," msemaji wa Taliban Suhail Shaheen ameliambia shirika la habari la AFP.

Ikiwa mazungumzo haya ya amani yaliyoahirishwa kwa muda mrefu, yatazaa matunda, hali hiyo itawezesha pia wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini Afghanistan kama ilivyoahidi Washington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.