Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-IS-TALIBAN-USALAMA

Watu 20 waangamia katika shambulio dhidi ya gereza Afghanistan

Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotokea katika gereza moja Mashariki mwa nchi ya Afghanistan, na kusababisha vifo vya watu karibu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 24.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan viapiga kambi karibu na eneo la shambulio la kujitoa mhanga huko Kabul, Afghanistan.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan viapiga kambi karibu na eneo la shambulio la kujitoa mhanga huko Kabul, Afghanistan. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutokea kwa shambulizi hilo, kulishuhudiwa kwa makabiliano makali kati ya washambuliaji na wanajeshi wa Afganistan katika mkoa wa Nangarhar.

Kundi la Islamic State, lenye tawi lake nchini humo limekiri kutekeleza shambulizi hilo wakati huu Umoja wa Mataifa ukisema kuwa nchi hiyo ina wapigani 2,200 wa kundi hilo.

Wakati hayo yakijiri kwa siku ya tatu kumeendelea kushuhudiwa hali ya utulivu kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan, huku mamia ya wafungwa wakiachiliwa huru kwa lengo la kuwezesha mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Tangu Ijumaa iliyopita, wakati wa Sikukuu ya Eid al-Adha, utulivu umeshuhidiwa nchini humo na hakuna mapigano yoyote yaliyoripotiwa.

Rais Ashraf Ghani na uongozi wa kundi la Taliban wamekubaliana kurudi tena kwenye meza ya mazungumzo hivi karibuni ili kupata amani ya kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.