Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA-USALAMA

Mlipuko mkubwa wasikika Kusini mwa Lebanon

Ghala la silaha la Hezbollah limeteketea kwa moto baada ya kutokea mlipuko mkubwa kufuatia "hitilafu ya kiufundi" , tukio ambalo limetokea Jumanne wiki hii katika kijiji cha Kusini mwa Lebanoni, chanzo kutoka idara za usalama kimebaini.

Lebanon inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mlipuko wa Agosti 4 katika bandari ya Beirut, ambao uligharimu maisha ya watu karibu 200, umezidi hali ya wasiwasi nchini humo.
Lebanon inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mlipuko wa Agosti 4 katika bandari ya Beirut, ambao uligharimu maisha ya watu karibu 200, umezidi hali ya wasiwasi nchini humo. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo umesababisha watu kadhaa kujeruhiwa, vyanzo kadhaa katika idara za usalama vimeongeza, bila hata hivyo kutoa takwimu sahihi.

Idhaa ya Hezbollah, Al Manar, imesema chanzo cha mlipuko huo hakijabainika.

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kishia nchini Lebanon wameweka vizuizi vya usalama karibu na eneo la tukio, katika kijiji cha Ain Qana, karibu kilomita 50 Kusini mwa mji wa Beirut, chanzo kingine kilicho karibu na idara za usalama kimesema. Wanahabari hawakuruhusiwa kufika eneo la tukio.

Hezbollah haijazungumza chochote kuhusiana na mlipuko huo.

Kusini mwa Lebanon ni ngome ya Hezbollah, kundi linaloungwa mkono na Iran ambalo linapigana huko Syria likisaidia vikosi vya serikali ya Damascus.

Lebanon inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mlipuko wa Agosti 4 katika bandari ya Beirut, ambao uligharimu maisha ya watu karibu 200, umezidi hali ya wasiwasi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.