Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA-USALAMA

Lebanon: Emmanuel Macron atangaza kuundwa kwa serikali mpya ndani ya siku 15

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchni Lebanon. Ziara iliyolenga kudumisha shinikizo kwa viongozi wa Lebanon ili waweze kuweka mageuzi yanayosubiriwa na jamii ya kimataifa.

Emmanuel Macron wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Residence Pine, huko Beirut, Septemba 1, 2020.
Emmanuel Macron wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Residence Pine, huko Beirut, Septemba 1, 2020. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa ametangaza kuwa vyama vyote vya kisiasa vimeahidi kwamba uundaji wa serikali mpya hautachukua zaidi ya siku 15.

"Vyama vyote vya kisiasa kwa kauli moja vimeahidi kwamba uundaji wa serikali inayozingatia majukumu yake hautachukua zaidi ya siku kumi na tano", amesema rais wa Ufaransa wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Beirut , baada ya mazungumzo na viongozi wakuu wa kisiasa.

Ameongeza kuwa serikali itaundwa na watu wenye "uwezo" na itaundwa "kama muungano huru ambao utapata uungwaji mkono na vyama vyote vya kisiasa".

Waziri Mkuu mpya, Moustapha Adib, aliyeteuliwa saa chache kabla ya kuwasili kwa rais Emmanuel Macron siku ya Jumatatu, anatarajia leo Jumatano kuanza mashauriano na bunge kwa minajili ya kuundwa kwa serikali hiyo mpya.

Rais wa Ufaransa amekumbusha kwamba "wastani katika miaka ya hivi karibuni" kwa kuunda serikali nchini Lebanon ilikuwa "kati ya miezi 5 na 11" kwa sababu ya tofauti za kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.