Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA-USALAMA

Lebanon: Macron atangaza misaada ya ziada na atoa wito wa kuundwa 'serikali yenye majukumu'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezuru bandari ya Beirut Jumanne asubuhi, huku chombo kiliokuwa kimesheheni msaada wa kibinadamu kutoka Ufaransa kikiwasili mapema leo asubuhi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awasili kwenye hafla ya upandaji mierezi na wajumbe wa shirika lisilo la kiserikali la Jouzour Loubnan huko Jaj, karibu na Beirut, Septemba 1, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron awasili kwenye hafla ya upandaji mierezi na wajumbe wa shirika lisilo la kiserikali la Jouzour Loubnan huko Jaj, karibu na Beirut, Septemba 1, 2020. REUTERS/Gonzalo Fuentes/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa ametaka kujionea mwenyewe hali halisi na mahitaji muhimu yanayotakiwa.

Wakati huo huo rais Macron ameendeleza kampeni yake ya kushinikiza mageuzi ya kisiasa nchini Lebanon wakati taifa hilo likitimiza miaka 100 ya uhuru wake.

Lebanoni inaendelea kukumbwa na mizozo mmbalimbali katikati mwa janga la Covid-19.

Macron alipowasili jana alisema mtazamo wake juu ya mfumo wa kisiasa nchini Lebanon haijabadilika na unabakia kuwa ''kuhimiza bila kuingilia''.

Macron, ambaye hii ni ziara yake ya pili nchini Lebanon tangu kutokea kwa mlipuko mkubwa uliosababisha vifo vingi katika bandari ya Beirut Agosti 4, ameendelea kuwataka viongozi wa Lebanon kuunda mara moja "serikali inayozingatia majukumu yake" ili kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro wa kiuchumi na kisiasa.

tayari nchi hiyo ina waziri mkuu mpya, Moustapha Adib, kutoka madhehebu ya Sunni.

Rais Emmanuel Macron anatarajia kuanza mazungumzo ya kisiasa na Rais Michel Aoun na wawakilishi wa vyama ambavyo viliteua Waziri Mkuu mpya, Moustapha Adib. Hali ambayo Emmanuel Macron anaiona kwa tahadhari wakati anataka kuweka shinikizo kwa wanasiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.