Pata taarifa kuu
IRAN-BAHRAIN-ISRAEL-UHUSIANO

Makubaliano ya kurejesha uhusiano: Iran yashutumu Bahrain kuwa 'mshiriki katika uhalifu' wa Israeli

Iran imeinyooshea kidole cha lawama Bahrain kwa kuwa sasa "msaidizi wa uhalifu" wa Israeli, siku moja baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Iran Hassan Rohani akiongoza mkutano wa serikali Mei 6, 2020 huko Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rohani akiongoza mkutano wa serikali Mei 6, 2020 huko Tehran. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Viongozi wa Bahrain sasa watahusishwa katika uhalifu wa utawala wa Kizayuni, kama tishio la mara kwa mara kwa usalama wa ukanda mzima wa Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu," wizara ya mambo ya nje ya Iran mesema katika taarifa.

Israeli na Bahrain zilifikia makubaliano ya kufufua uhusiano wao Ijumaa (Septemba 11), mwezi mmoja baada ya makubaliano kati ya Falme za Kiarabu na nchi hiyo ya Kiyahudi.

Katika taarifa ya pamoja, Marekani, Bahrain na Israeli zimesema kuwa kufungua mawasiliano ya moja kwa moja na ushirikiano kati ya pande hizo mbili na chumi zilizoimarika kutaendelea kuleta mabadiliko ya manufaa katika eneo la Mashariki ya Kati na kuongeza uthabiti, usalama na ufanisi katika eneo hilo.

Ikulu ya White House nchini Marekani imesema rais Donald Trump alitoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al Khalifa na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.Akiwahutubia wanahabari katika ofisi yake, Trump aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria na kwamba anaamini mataifa mengine yatafuata mkondo huo.

Mwezi uliopita, Umoja wa Falme za Kiarabu ulikubali kurejesha uhusiano wa kawaida na Israel chini ya mkataba uliosimamiwa na Marekani unaotarajiwa kutiwa saini katika sherehe itakayoandaliwa katika ikulu ya White House siku ya Jumanne, itakayoongozwa na rais Trump anayetafuta kuchaguliwa tena kama rais katika uchaguzi wa Novemba 3. Sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Falme za Kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed al-Nahyan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.