Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-UNSC-USALAMA

Azimio la Marekani kuhusu kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran latupiliwa mbali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefutilia mbali azimio kuhusu vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran kuhusiana na suala la nyuklia. Azimio hilo lililowasilishwa na Marekani, lililenga kurefusha bila kikomo vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huko New York.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, huko New York. Stephane LEMOUTON / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo jipya lililowasilishwa na Marekani linataka vikwazo hivyo kurefushwa bila ya kikomo ikisema iwapo vitaondolewa, Iran itakuwa msambazaji wa silaha bila kuzingatia maadili ya kimataifa.

Hata hivyo Marekani imetishia kurejesha vikwazo vilivyochukuliwa kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa mwaka 2015.

Marekani imesema hatua hiyo itakomesha ufedhuli wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Marufuku iliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015 ya kuingiza au kuuza silaha zote za kivita kwa Iran inatarajiwa kufikia mwisho Oktoba 18 mwaka huu.

Rais wa Iran Hassan Rouhani alikuwa ameonya kuwa nchi yake ingejibu iwapo Baraza la Usalama lingerefusha vikwazo hivyo vya silaha lakini hakuainisha hatua watakazochukuwa.

Makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran, Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Marekani yalianza kuyumbayumba baada ya Marekani kujitoa na Tehran kuanza kukiuka vipengele vya mkataba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.