Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Syria: Waasi wanaoungwa mkono na Ankara wadhibiti mji ulio karibu na Idlib

Waasi wa Syria wanaoungwa mkono na jeshi la Uturuki wamedhibiti mji wa Narab, katika mkoa wa Idlib, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Uturuki na wawakilishi wa waasi.

Gari za jeshi la Uturuki zinaonekana katika mji wa Binnish katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Syria wa Idlib, karibu na mpaka wa Syria na Uturuki Februari 12, 2020.
Gari za jeshi la Uturuki zinaonekana katika mji wa Binnish katika mkoa wa kaskazini magharibi mwa Syria wa Idlib, karibu na mpaka wa Syria na Uturuki Februari 12, 2020. Muhammad HAJ KADOUR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya rais Bashar al-Assad, ambavyo vinaungwa mkono na jeshi la anga la Urusi, wanajaribu kuiteka ngome hii ya mwisho ya waasi nchini Syria baada ya miaka tisa ya vita.

Karibu raia milioni moja wameyahama makazi yao tangu kuanza tena kwa mashambulizi ya vikosi vya serikali vya Syria na mshirika wake Urusi Desemba mwaka jana, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Vikosi vya serikali vimeuteka mji wa Kafr Nabel na maeneo jirani, yanayopatikana karibu kilomita 30 Kusini Magharibi mwa Nairab, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), chanzo cha eneo hilo na vyombo vya habari vimeripoti.

Ankara imetuma maelfu ya askari na vifaa katika mkoa huo kusaidia waasi wa Syria, na kuongeza mvutano na Moscow, mshirika mkuu wa Damascus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.