Pata taarifa kuu
ISRAELI-SYRIA-GAZA-USALAMA

Israeli yakiri kufanya mashambulizi nchini Syria na Gaza dhidi ya kundi la Islamic Jihad

Hatimaye, Israeli imesema imetekeleza shambulio la anga nchini Syria, Kusini mwa mji mkuu wa Damascus dhidi yangome za kundi la Islamic Jihad.

Israel yatekeleza mashambulizi ya anga Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 23, 2020.
Israel yatekeleza mashambulizi ya anga Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 23, 2020. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Haya ni matokeo ya Jumapili Februari 23 kutoka kwenye mpaka kati ya Israeli na Gaza, Israeli imesema katika taarifa. Watu sita waliuawa katika shambulio hilo, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) limebaini.

Jeshi la Israeli limethibitisha kutekeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya ngome mbalimbali za kundi la Islamic Jihad nchini Syria.

"Jeshi la Israeli limejibu na limetekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya ngome za magaidi katika eneo la Gaza na karibu na mji wa Damascus nchini Syria. Hii ni pamoja na maeneo ya kutengeneza, miundombinu ya ardhini kunakopatikana kiwanda cha kutengeneza roketi, na kituo cha mafunzo, "Luteni Kanali Jonathan Conricus, msemaji wa jeshi la Israeli amesema.

Mapigano baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Islamic Jihad yalishamiri mwezi wa novemba, wakati mashambulio ya anga ya Israeli yalipomuua kamanda wa ngazi yajuu wa kikundi cha wanamgambo mjini Gaza.

Makabiliano baina ya vikosi vya Israeli na Wapalestina yalishuhudiwa mapema mwezi huu pia, siku moja baada ya rais wa Marekani Donal Trump kutangaza mpango wake wa amani, na kufungua ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.