Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Watu 900,000 wahama makazi yao kufuatia ghasia kaskazini magharibi mwa Syria

Watu 900,000 hawana makao Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Syria, tangu mwezi Desemba mwaka uliopita kutokana na operesheni dhidi ya makundi ya waasi.

Tangu Desemba, watu 900,000 nchini Syria wamelazimika kuyahama makazi yao kufuati machafuko Kaskazini Magharibi mwa nchi.
Tangu Desemba, watu 900,000 nchini Syria wamelazimika kuyahama makazi yao kufuati machafuko Kaskazini Magharibi mwa nchi. RAMI AL SAYED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, idadi ya watu hao ni wanawake na watoto ambao wengi pia wanapoteza maisha kwa sababu ya baridi kali katika kambi ambazo zimejaa.

Idadi hii imeongezeka maradufu, baada ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni kusema kuwa watu waliokuwa wamekimbia makwao katika jimbo hilo la Idlib ni 100,000.

Jeshi la Urusi linaongoza mashambulizi dhidi ya makundi ya waasi na hatua hiyo imesababisha idadi kubwa ya watu kukimbia makwao katika jimbo hilo, kwa kipindi kifupi.

Mapigano nchini Syria yamekuwa yakiendelea tangu mwaka 2011, kwa makundi ya waasi kumtaka rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani, vita ambavyo vimesababisha vifo vya watu 380,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.