Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA-SIASA

Syria: Vikosi vya serikali vyasonga mbele Kaskazini-Magharibi, raia 17 wauawa

Vikosi vya serikali ya Syria, vikisaidiwa na Urusi, vimesonga mbele katika mji muhimu katika Mkoa wa Idleb kutokana na mashambulizi kabambe dhidi ya mkoa huo wa Kaskazini-Magharibi mwa nchi inayoendelea kukumbwa na vita, ambapo raia 17 wakiwemo watoto waliangamia katika mashambulizi jana Alhamisi.

Wakaazi wa Binnish wachoma moto matairi kuzuia mashambulizi  ya anga ya serikali ya Syria Februari 6, 2020 katikaMkoa wa Idleb.
Wakaazi wa Binnish wachoma moto matairi kuzuia mashambulizi ya anga ya serikali ya Syria Februari 6, 2020 katikaMkoa wa Idleb. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na janga hilo la kibinadamu lililosababishwa na mashambulizi hayo, ambalo lilizinduliwa tena mwezi Desemba dhidi ya mkoa wa Idleb na maeneo jirani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana kwa haraka huko New York siku ya Alhamisi kwa ombi la Marekani, Ufaransa na Uingereza.

Nchi za Magharibi zimelaani vikali "mauaji" yanayoendelea katika mkoa huo, huku nchi kadhaa hasa za Ulaya zimetoa wito wa "kukomesha mapigano". Kwa upande wake, Iran kupitia balozi wake katika Baraza la Usalama la Umpja wa Mataifa limependekeza kutoa msaada wake ili kupunguza mvutano kati ya Syria na Uturuki.

Na "kuna mahitaji ya dharura endelevu na ya haraka kwa raia," amesema Geir Pedersen, mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria.

Ndani ya kipindi cha miezi miwili, takriba watu 586,000 wamelazimika kuyatoroka makaazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea katika mkoa huo, ambao nusu yake inadhibitiwa na wapiganaji wa kijihadi na ambapo makundi ya waasi yamepiga kambi, kulingana na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Uturuki, ambayo ina wanajeshi Kaskazini Mashariki mwa Syria pamoja na Idleb, ambapo inasaidia waasi, imeimtaka mara kadhaa Bashar al-Assad na Moscow kusitisha mashamblizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.