Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-UNSC-USALAMA

Machafuko Gaza: Marekani yapinga shutma dhidi ya Israel

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kukutana kwa dharura Jumanne wiki hii kwa ombi la Kuwait kufuatia machafuko yaliyozuka katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na karibu 1,600 waliojeruhiwa.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley (picha ya kumbukumbu).
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Wapalestina wanataka kusikia Umoja wa Mataifa ukishtumu mauaji hayo na wanaomba uchunguzi huru na wa wazi kuhusu kuhusika kwa majeshi ya Israeli katika mauaji hayo, lakini Marekani inapinga.

Wanadiplomasia hawawezi kubaki kimya kufuatia machafuko ya siku ya Jumatatu, machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wengi tangu kuanza kwa maandamano katika Ukanda wa Gaza Machi 30. Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea masikitiko yake, na haja ya kuzindua uchunguzi huru na wa wazi ili wahalifu wakabiliwe na mkono wa sheria.

Taarifa hiyo ilikuwa na lengo la kuelezea "ghadhabu na [huzuni] [ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa] dhidi ya vifo vya raia wa Palestina ambao walikua na haki ya kuandamana kwa amani".

Lakini Marekani, kama inavyofanya kwa wiki saba zilizopita, imekapinga shutma hizo dhidi ya Israeli, na hivyo kuzuia tamko lolote rasmi la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tangu mgogoro huo kuanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.