Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Trump kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa katika saa chache zijazo kutangaza kutambua mji wa Jerusalem, kuwa makao makuu ya Israel na kuanza harakati za kuhamisha ubalozi wake kutoka mjini Tel Aviv.

Ubalozi wa Marekani Tel Aviv.
Ubalozi wa Marekani Tel Aviv. JACK GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Trump anatarajiwa kutoa tangazo hili baadaye hivi leo ambalo tayari limewakasirisha viongozi wa Palestina na kutoka mataifa ya kiarabu.

Viongozi hao wa mataifa ya Kiarabu wamesema hataua hiyo ya Marekani itakuwa na madhara makubwa na ni uchokozi kwa Waislamu.

Mfalme wa Jordan Abdullah na rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi wamesema hatua hiyo itasabisha ukosefu wa udhabiti katika eneo la Mashariki ya Kati

Ripoti zinasema kuwa tayari rais Trump amewapigia simu viongozi wa mataifa ya kiarabu na kuwaambia hatua ya serikali yake.

Aidha, Trump anatarajiwa kuiagiza Wizara ya Mambo ya nje, kuhamisha Ubalozi wake kwenda Jerusalem, hatua ambayo hata hivyo itachukua miaka kadhaa.

Mji wa Jerusalem umeendelea kuaminiwa na Waisraeli na Wapelestina kama mji Mtakatifu, huku Israel ikisema ndio mji wao Mkuu lakini Palestina nayo ikisema Mashariki mwa mji huo wa Jerusalem ndio Makao makuu ya nchi yao katika siku zijazo.

Marekani inakuwa nchi ya kwanza duniani, kutambua Jerusalem katika mji mkuu wa Israel tangu kuundwa kwa taifa hilo mwaka 1948.

Hata hivyo hatua hiyo itakua haina uzito wowote, kwani itakua tu ni kama kukamilisha ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake katika uchaguzi wa urais. Mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani katika mji wa Jerusalem kutoka Tel Aviv unaweza ukachkua muda wa miaka minne, kwa mujibu wa wadadisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.